KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Tuesday, August 23, 2016

BANK OF AFRICA YAFUNGUA TAWI LA KISASA MKOANI MANYARA.

 Meneja wa Bank of Africa (BOA), tawi la Babati, Goodluck  Mwasa akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tawi hilo.
Meneja wa Bank of Africa  (BOA), tawi la Babati, Goodluck  Mwasa (kulia), akifafanua jambo kwa Kamishna wa Polisi wa Mkoa  wa Manyara, Francis Massawe. Wa pili kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank  of Africa, Ammishaddai Owusu-Amoah akitoa hotuba fupi kwenye hafla ya uzinduzi  wa tawi la Babati mkoani Manyara.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino  Kazimoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Ammishaddai Owusu-Amoah na Meneja  wa Tawi jipya la Babati, Goodluck Mwasa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Longino Kazimoto akikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa tawi jipya la Bank  of Africa mjini Babati.
Waliokaa kutoka kushoto ni  Samson  Ntunga, akimuwakilisha Katibu Tawala (Manyara), Mkurugenzi Mtendaji wa wa Bank of  Africa,  Ammishaddai Owusu-Amoah akiwa na mgeni rasmi, Longino Kazimoto  na RPC Franc
  
Na Mwandishi Wetu

 MKUU wa Mkoa wa Manyara,  Joel  Bendera, amesema  maendeleo ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini hayawezi kuwa na mafanikio bila ya kuhusisha Sekta binafsi.
Bendera alitoa kauli hiyo, mwishoni mwa wiki katika sherehe za ufunguzi wa matawi mapya ya benki  ya Tanzania yaliyofunguliwa,  Babati mkoani Manyara.

Alisema  Benki  hiyo  imedhamiria kupanua shughuli za kibenki nchini hasa katika kukuza uchumi wa watu  wa  Babati.
“Benki  hii  inakuja na mengi mapya katika Sekta ya Benki na kuleta huduma za kibenki karibu na wananchi wa Babati   ikiungana na Benki zingine pamoja na kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania,”alisema  Bendera na kuongeza “Niombe uongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Benki ya  Afrika kuhakikisha kwamba wateja wa tawi la Babati wanapata huduma za kipekee katika viwango vya kimataifa tukiweka pamoja na mahitaji ya wana Babati katika benki yenu. natumaini kuwa una wafanyakazi wenye sifa, uwezo na weledi wa kufanya kazi na hivyo unachohitaji sasa ni wateja,”alisema  Bendera.

Bendera alisema Serikali inafanya kila iwezalo katika kuhakikisha huduma za kifedha zinamfikia kila mwanachi kwa urahisi na kwamba  katika kuhakikisha hili linafanyika serikali itaboresha miundombinu hasa barabara, njia za mawasiliano na utengenezaji wa Sera zilizo stahiki na kupigana na umasikini.

Aliongeza  kuwa Serikali itaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuhamasisha wawekezaji zaidi Nchini.

“ Pamoja na jitihada hizo bado kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kujenga mazingira bora ya Sekta Binafsi kukua hasa suala la upatikanaji wa huduma za Kibenki Vijijini na katika Sekta ya Kilimo,”alisema Bendera.

No comments: