KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, September 22, 2016

KAMPENI YA KUCHANGIA MADAWATI YA 'SIMAMA KAA CAMPAIGN' YAZINDULIWA.

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Dk. Amon Foundation, Amon Mkoga leo ametoa mchango wa madawati katika kampeni ya uchangiaji madawati kwa udhamini wa mtandao wa simu za mkononi wa Halotel Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Amon Mkoga amesema kuwa katika kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli wameandaa kampeni ya maalum ya "Simama Kaa Desk Campaign" itakayosaidia kupunguza uhaba wa madawati uku ikidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel.

Aidha amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuchangia na kupunguza upungufu wa madawati katika shule mbalimbali za msingi na sekondari ili kuunga mkono jitahada za Rais Magufuli, kampeni hiyo itaanzia katika mkoa wa Tabora na Pwani.

Ofisa Mawasiliano wa Halotel, Stella Pius amesema kuwa Halotel itakuwa pamoja na Dk. Mkoga Foundation kuhakikisha kwamba watakuwa bega kwa bega ili kuwasilisha mchango wa madawati katika elimu pamoja na kuunga mkono uchangiaji wa madawati.
 Mwenyekiti wa taasisi ya Dk. Amon Mkoga, Amon Mkoga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uzindua wa mradi wa ‘Simama Kaa Desk Campaign' wenye lengo la kushirikiana na serikali kugawa madawati katika shule zenye upungufu. Kushoto ni Meneja Masoko wa Halotel, Ngo Duy Truong na Ofisa Mahusiano wa Halotel, Stella Pius. (Picha na Francis Dande)
 Mwenyekiti wa taasisi ya Dk. Amon Mkoga, Amon Mkoga (katikati), Meneja Masoko wa Halotel, Ngo Duy Truong (kushoto) na Ofisa Mahusiano wa Halotel, Stella Pius wakizindua mradi wa ‘Simama Kaa Desk Campaign wenye lengo la kushirikiana na serikali kugawa madawati katika shule zenye upungufu.
 Mwenyekiti wa taasisi ya Dk. Amon Mkoga, Amon Mkoga (katikati), Meneja Masoko wa Halotel, Ngo Duy Truong (kushoto) na Ofisa Mahusiano wa Halotel, Stella Pius wakizindua mradi wa ‘Simama Kaa Desk Campaign wenye lengo la kushirikiana na serikali kugawa madawati katika shule zenye upungufu
Waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi huo.

No comments: