KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, November 30, 2016

UNESCO-TANZANIA YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA KUTOKAWIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KATIKA KUTEKELEZA MPANGO MKAKATI WA WIZARA MAWAKA 2016/2017.

 Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), nchini Tanzania, Zulmira Rodrigueas, (kulia), akiendesah semina ya mafunzo ya siku tatu kujenga uwezo kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, makao makuu ya UNESCO, Oysterbay jijini Dares Salaam, leo Novemba 30, 2016. Kushoto ni Mwanasheria wa Wizara, Evordy Kyando.

NA K-VISBLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni , (UNESCO), limeendesha mafunzo ya siku tatu kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ili kuwajengea uwezo wa kutekeelza mpango mkakati wa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 30, 2016, na kuendeshwa na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, nchini, Bi. Zulmira Rodrigues yanafanyika kwenye ofisi za shirika hilo, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Tumekusanyika hapa kwa mara ya kwanza kuisaidia wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuboresha uwezo wawafanyakazi wake, wafanyakzi kutoka idara tofauti tunao hapa, wapo kutoka idara ya Habari, Utamaduni, michezo pamoja na idara za kiusaidizi kama vile fedha, sheria, ICT na kadhalika.” Alianza kwa kusema Mkuu huyo wa UNESCO.
Alisema, Mpango unaweza kusaidia kufanya tathmini na marekebisho kwa mahitaji ya wizara au taasisi yoyote ile na kwa kuzingatia hilo, Shirika hilo limeona upo umuhimowa kuwajengea uwezowatendaji katika wizara hiyo ili kutekeleza vema mpango mkakati wa wizara. “Kama huna mpango wowote ule uliouweka, utajikuta unatumia nguvu nyingi na kuishia patupu bila mafanikio yoyote yale.” Alisema.
Alisema, wafanyakazi katika taasisi yoyote ile ni wajibu kushirikiana ili kuwa na lengo moja kufikia malengo mahsusi yaliyopangwa na Wizara au taasisi. “Kabla ya kuweka mpango wowote ni lazima kufanyike utafiti wa hali halisi ya jambo linalotaka kushughulikiwa.” Alifafanua Bi. Zulmira.
Washiriki walianza kujifunza mambo mbalimbali ama vile, namna ya kutambua tatizo la msingi, uwezo, udhaifu, fursa na tishio mambo yote hayo yanayojulikana kitaalamu kama (SWOT Analysis), ndiyo yatakayotoa picha halisi ya namna ya kupanga mkakati na namna ya kuutekeleza mkakati huo.


Aidha washiriki wa warsha hiyo wamefurashiswa na mafunzo hayo kwani yatasaidia kuwajengea uwezo wa kutekeelza kikamilifu malengo ya kiofisi na binafsi.
“Mafunzo haya yatanisaidia sana katika kutekeleza malengo yaliyopangwa kwani nimejifunza njia mbalimbali za kimkakati katika kutekeleza malengo yaliyopo.” Amesema mshiriki Lorietha Lawrence, afisa habariwizara ya Habari, Utamaduni, Sanaana Michezo.
Kupitia mafunzo haya, ninahakika yatasaidia kutekelza majukumu yangu ya kila siku, na nitakachojifunza nitashirikiana na wenzangu kwenye kitengo chetu katika kutekelezaipasavyo majukumu yetu.” Alisema Afisa mwingine wa habari, Lilian.
 Baadhi ya washiriki
Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, Sefania Molela, akizungumza
 Mshiriki kutoka idara ya Habari akizungumza
 Bi. Zumlira Rodrigues, (kulia), akiteta jambo na Afisa Mpango wa Utamaduni wa UNESCO, Rahma Sudi
 Afisa Mpango wa UNESCO, Michaela Konopikova
 Mtaalamu wa masuala ya ICT wa UNESCO, Leonard Kisenha, (katikati), na Afisa Mpango, Utamaduni wa Shirika hilo, Michaela, (kushoto0, wakitazama kitu kwenye kompyuta
 Mkufunzi wa UNESCO, Deirdre Prins-Solan
 Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, akizungumza

 Mshiriki kutoka idara ya Michezo akizungumza
 Zulmira akiendesha mafunzo
 Maafisa mpango-Utamaduni wa UNESCO, Rehema (kulia) na Michaela wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo
 Zulmira akiendesha mafunzo
Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Evordy Kyando, akizungumza jambo

No comments: