KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Saturday, March 25, 2017

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AWAONDOA HOFU WANACHAMA WA PPF KUFUATIA UAMUZI WAKE WA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 26 wa Wamachama na Wadau wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), jijini humo Machi 24, 2017. Kauli mbiu ya Mkutano huo ilikuwa, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”.
Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Waziri alisema"Naomba niwatoe hofu Wanachama wa PPF, kuhusu uamuzi wa Mfuko kuwekeza kwenye viwanda, kwani uamuzi huu ni sahihi kwa sasa, ikizingatiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda, lakini pia Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kujenga uchumi wa viwanda." Alitoa hakikisho Waziri Mhagama.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw.William Erio, akionyesha furaha yake kufuatia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika mkutano huo ambapo alisema, jumla ya washiriki 800 walihudhuria mkutano huo na hivyo Mfuko umefanikiwa kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa, akizungumza kwenye mkutano huo. Yeye alisema Jeshi la Magereza limeamua kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo PPF na NSSF katika kutekeleza mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na PPF, wanafanya uwekezaji mkubwa katika kiwanda cha viatu kule gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro na kwenye kiwanda cha sukari kwenye shamba la Mbigiri mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, akifuatilia kwa makini mkutano huo

No comments: