Makamu
wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Ramadhan Nassib ametoa sh. milioni moja kwa waamuzi waliochezesha mechi
ya Simba na Yanga iliyochezwa wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam.
Nassib
ambaye alichaguliwa katika nafasi hiyo akiwakilisha klabu amesema
ametoa fedha hizo ili kuwapongeza waamuzi hao kwa kuchezesha vizuri
mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3.
“Waamuzi
wanapofanya vibaya tunawaadhibu, hivyo wakifanya vizuri wanastahili
kupongezwa pia. Vilevile kuwapongeza ni kuwaongezea ari ya kuchezesha
vizuri zaidi,” amesema.
Israel
Nkongo ndiye aliyeongoza jopo hilo ambapo mwamuzi msaidizi namba moja
alikuwa Hamis Chang’walu wakati namba mbili alikuwa Ferdinand Chacha.
Mwamuzi wa mezani alikuwa Oden Mbaga.
Waamuzi
wote hao wana beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA),
na watoka Dar es Salaam ukiondoa Chacha ambaye maskani yake ni Bukoba
mkoani Kagera.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment