Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma akipokewa na
ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa siku mbili baina ya Afrika na
Ulaya mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Sheraton huko Brussels
nchini Ubelgiji akitokea nchini Uingereza.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenza wa
mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Ubelgiji.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Madagascar
Mama Lalao Rajaonarimampianina muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye
chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa Afrika kwa
ajili ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano
wa Afrika na Ulaya unaofanyika huko Brussels.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadaye wakibadiishana
mawazo na Mke wa Rais wa Congo Mama Antoinnethe Sassou Nguesso wakati wa
hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Jumuia ya wenza wa
mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao huko Ubelgiji.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Cameroon
Mama Chantal Biya muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye chakula cha
mchana walichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika
wanaowakilisha nchi zao huko Ubelgiji kwenye hoteli ya Sheraton.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea cheti maalum cha ulezi wa
heshima wa Chama cha wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika walioko nchini
Ubelgiji (Honory Patronese of the Association of the Spouses of African
Ambassadors in Belgium) kutoka kwa Mke wa Balozi wa Cameroon nchini
Ubelgiji Mama Christiane Eloundov de Evina wakati wa chakula cha mchana
walichowaandalia wake wa Marais wa Afrika jijini Brussels.

Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mama Adelaida Kamala
akimkabidhi Cheti Maalum cha ulezi wa heshima cha wenza wa mabalozi wa
Afrika walioko Ubelgiji, Mke wa Rais wa Cameroon Mama Chantal Biya
wakati wa chakula cha mchana walichowaandalia wageni hao kwenye hoteli
ya Sheraton.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake
wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika pamoja wa wenza wa Mabalozi wa
nchi hizo mara baada ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na
wenza hao.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
Na Anna Nkinda – Brussels, Ubelgiji
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amepewa cheti na
Umoja wa wake wa Mabalozi wa Afrika waishio katika nchi za Jumuia ya
Ulaya kwa kutambua na kuthamini mchango wake na kazi anazozifanya za
kuwasaidia wanawake, wasichana na watoto wa Tanzania.
Cheti hicho amekabidhiwa jana katika hafla fupi ya chakula
cha mchana kilichoandaliwa na wake hao wa mabalozi katika ukumbi wa
mikutano uliopo Hoteli ya Sheraton mjini Brussels.
Mama Kikwete ni mmoja kati ya wake wa Marais wa tano wa
Afrika waliokabidhiwa vyeti hivyo vya heshima kutokana na kazi zao
wanazozifanya za kuisaidia jamii na kuhakikisha kuwa inapata mahitaji ya
muhimu kama huduma ya afya na elimu.
Akiongea kabla ya kuwakabidhi wake hao wa marais vyeti
hivyo Mke wa Balozi wa Equatorial Guinea ambaye pia ni rais wa umoja
huo Mama Mangue de Nvono Nca alisema nia ya kuanzishwa kwa umoja wao ni
kulitambulisha bara la Afrika ambalo linajulikana kuwa na changamoto
za njaa, magonjwa, kutokuwa na haki na usalama wa kutosha katika nchi
za Ulaya.
“Siyo kama Bara letu la Afrika linakabiliwa na changamoto
peke yake bali pia limejaliwa kuwa na umoja, mshikamano na ukarimu na
haya yote yamejidhihirisha kwetu leo hii kutokana na kitendo cha wake
wa marais wetu kushiriki pamoja nasi katika hafla hii na kubadilishana
mawazo”, alisema Mangue de Nvono Nca.
Alisema umoja huo unatambua kazi kubwa inayofanywa na wake
wa Marais wa Afrika kwa jinsi wanavyowaunga mkono wenza wao kwa
kufanya kazi ambazo malengo yake makubwa ni kuwasaidia wanawake,
wasichana , watoto na watu ambao wako katika makundi hatarishi ndani ya
jamii.
Akiongea kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutunukiwa
vyeti hivyo Mke wa Rais wa Congo Brazzavile Mama Antoinette N’Guesso
aliwashukuru wake hao wa mabalozi kwa kazi wanayoifanya ya kulitangaza
bara la Afrika kuwa ni nchi ya umoja, mshikamano na ukarimu jambo ambalo
litaondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa kitu pekee kilichopo
barani Afrika ni matatizo.
Wengine waliokabidhiwa vyeti hivyo ni pamoja na Malkia wa
Swaziland Inkhosikati Zena Seraya Mahlangu , Mke wa Rais wa Madagascar
Mama Lalao Rajaonarimampianina, Congo Brazzaville Mama Antoinette
N’Guesso na Cameroon Mama Chantal Biy.
Wake hao wa Marais wameambatana na wenza wao ambao ni
Marais wa Afrika wanaohudhuria mkutano wa nne wa wakuu wa nchi za
Afrika na Jumuia ya Ulaya unaofanyika nchini humo.
No comments:
Post a Comment