Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwa ajili
ya ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya mpya ya Kalambo, Ofisi
hiyo ipo mji mdogo wa Matai mkoani Rukwa jana. Kinana yupo katika mkoa
wa Rukwa kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama, Utekelezaji wa ilani ya
chama na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzipatia
ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanga matofali baada ya
kushshiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya
mpya ya Kalambo, Ofisi hiyo ipo mji mdogo wa Matai mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana akiondoka kwenye Ofisi ya CCM wilaya mpya ya
Mkalamo baada ya kushiriki ufyatuaji matofali kwa ajili ya kuboresha
jengo la ofisi hiyo. Watatu kulia ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume
ambaye amefuatana na Kinana katika ziara ya mkoa wa Rukwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa shina namba
moja, Apolinary Kibiko, alipofika kwenye shina hilo, katika kijiji cha
Matai, wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano
uliofanyika kwenye shina namba mbili la mjumbe, Daudi Nkaisi (kushoto),
katika mji mdogo wa Matai, wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Mbunge
wa Kalambo Josephat Kandege akisalimia wananchi, Kinana alipowasili
katika shina namba mbili, katika Kijiji cha Matai, wilaya mpya ya
Kalambo.
Wananchi
wakishangilia Kinana alipozungumza nao kwenye shina namba moja, katika
Kijiji cha Matai wilaya ya Kalambo.
Wananchi wakimshangilia Kinana alipozungumza nao kwenye shina namba mbili katika kijiji cha Matai
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia ukumbini kuzungumza na wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Msafara
wa Kinana ukienda Kijiji cha Kasanga kilichopo mwambao wa ziwa
Tanganyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa,
Wananchi
wakijimwayamwaya kwenye mkutano wa Kinana uliofanyika kijiji cha
Kasanga, wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Kinana
akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kasanga kilichopo
mwambao wa ziwa Tanganyika katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Mabinti
wa kijiji cha Kalambo kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika, wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa akifurahia kurekodi matukio ya mkutano wa Kinana
kwa kutumia simu zao, alipohutubia katika kijiji hicho.Licha ya kuwa pembezoni Kijiji cha Kalambo ni miongoni mwa vijiji
vinavyopata mtandao wa mawasiliano ya uhakika ya simu za mkononi.
Mama akimyanyua mtoto wake apate kumuona Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kalambo.
Kijana
Ramadhani Ali wa Kijiji cha Kasanga kilichopo mwambao wa ziwa
Tanganyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa akitoka ziwani na
samaki wake aina ya migebuka.(Picha zote na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment