KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Sunday, July 28, 2013

UJENZI WA MSINGI NGUZO ZA DARAJA LA KIGAMBONI UNAKARIBIA KUMALIZIKA .

Moja ya nguzo kubwa ya 8 kati ya 13 zikiwepo na ndogo zitakazojengwa katika Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 ikiendelea kujengwa katika kina kirefu cha maji yaliyoondoshwa na kuzunguka pembeni, ili kutoa nafasi kwa wataalamu kufanya kazi yao.
Mafundi Vibarua kama wanavyojiita wenyewe wakiendelea na kazi ya kuchomea moja ya nguzo ndogo eneo la Ujenzi Vijibweni.
 Nguzo kubwa ikiwa katikati ya kina kirefu cha maji.
Mhandisi,Karim Mattaka,wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akifuatilia kwa karibu Ujenzi wa moja ya nguzo ya 8 iliyozungukwa na maji inayoonekana sehemu ya chini baada ya maji kuwekwa pembeni.
 Nguzo zinazoendelea kukamilika zikiendelea kukamirishwa.
 Mafundi wa Kichina na wetu (kulia) wakiangalia nguzo ya 8.
 Sehemu ya wafanyakazi Vibarua kama wanavyojiita wenyewe wakiwa mzigoni.
 Mabomba ambayo yatazamishwa chini ya ardhi kwenye maji yakisubiri kuzamishwa
 Mhandisi,Karim Mattaka,akionesha moja ya nguzo ndogo yenye nondo zaidi ya mia moja (100---) ambayo inakaribia kumalizika upande wa Kurasini.
 Nondo zilizosukwa pamoja zimeandaliwa kujengewa nguzo. 
 Baadhi ya Wananchi wanaoishi maeneo ya Vijibweni na kwengineko wakianza kunufaika kwa kutumia kwa magari na waendao kwa miguu kuvuka katika Daraja linalotumika kupitishia vifaa vya ujenzi wa Daraja.
 Gari la Polisi likipitishwa  katika Daraja la muda kuelekea Vijibweni.
 Fundi wa Kichina akichomea nondo zinazoumba nguzo za daraja.
Mafundi vibaru wazawa wakionesha viatu walivyonunua kutoka kwa wachina kwa Tsh.20,000 kwa ajili ya kufanyia kazi ili kulinda usalama wao, Pia wamedai hawalipwi vizuri,fundi wa kawaida analipwa Tsh.5000 kwa siku na fundi wa juu Tsh.6000 na 8000 kwa fundi mkubwa Mzawa.
Vibarua wakiendelea kuchapa kazi katika eneo la Ujenzi wa Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita  680 linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

No comments: