JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
|
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(CSEE) ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
1.0
UTANGULIZI
Mtihani wa Kidato cha Nne, 2012 ulifanyika
nchini kote kuanzia tarehe 8/10-25/10/2012. Baraza la Mitihani la
Tanzania katika kikao chake cha 94 kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2013 liliidhinisha
matokeo haya
2.0
USAJILI
NA MAHUDHURIO
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika
katika kufanya mtihani huo ikilinganishwa na vituo 4,795 vilivyotumika mwaka 2011.
2.1
Taarifa
za Watahiniwa
Jumla ya watahiniwa 480,029 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato
cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,587 sawa na asilimia 45.33 na
wavulana 262,442 sawa na asilimia 54.67. Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni 458,139
sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa
21,890 sawa na asilimia 4.56 ya watahiniwa wote waliosajiliwa,
hawakufanya mtihani.
2.2
Watahiniwa
wa Shule
Watahiniwa
wa shule waliosajiliwa ni 411,225 wakiwemo
wasichana 182,982 sawa na asilimia 44.50
na wavulana 228,243 sawa na asilimia
55.50. Watahiniwa wa shule
waliofanya mtihani walikuwa 397,138 sawa na asilimia 96.57.
Aidha, watahiniwa 14,087 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo
utoro, ugonjwa na vifo.
2.3
Watahiniwa
wa Kujitegemea
Watahiniwa
wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni
68,804 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.30 na wavulana 34,199
sawa na asilimia 49.70.
Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,918 na wavulana 30,083 wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,803
sawa na asilimia 11.34 hawakufanya mtihani.
3.0
MATOKEO YA MTIHANI
3.1
Maandalizi
ya matokeo
Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Nne mwaka 2012 yalitangazwa tarehe 18 Februari 2013 na kufutwa Machi 2013
kutokana na sababu za kitaalamu katika matumizi ya taratibu za kuchakata
matokeo. Matokeo yaliyofutwa yalikuwa yamechakatwa kwa kutumia utaratibu wa
Fixed Grade Ranges. Matokeo yanayotangazwa sasa yamechakatwa kwa utaratibu huo
huo lakini yamefanyiwa Standalization.
Kimataifa kuna aina kuu mbili za kuchakata matokeo
ya mtihani : Flexible ‘Grade Ranges na Fixed Grade Ranges’.
‘Flexible Grade Ranges’ hutumia viwango tofauti
kuchakata matokeo ya watahiniwa kwa kuzingatia kiwango cha ufaulu cha somo
husika kwa kila mwaka. Hivyo viwango vya kuchakata matokeo hubadilika kila
mwaka kulingana na ufaulu wa watahiniwa kwa kila somo husika.
Katika mfumo wa ‘Fixed Grade Ranges’ viwango vya
aina moja hutumika kuchakata matokeo kwa masomo yote bila kujali kiwango cha
kufaulu kwa somo husika. Viwango vya kuchakata matokeo hutumika hivyo hivyo
kila mwaka bila mabadiliko.
Kwa miaka mingi Baraza la Mitihani la Tanzania
limekuwa likitumia mfumo wa ‘Flexible Grade Ranges’. Mwaka 2012, mfumo wa
‘Fixed Grade Ranges’ ulitumika kuchakata matokeo kwa mara ya kwanza
Mabadiliko hayo yalitokana na maoni ya wadau
yaliyotokana na utafiti uliofanywa na Wizara mwaka 2010 kufuatia kushuka kwa
ufaulu wa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huo. Pia kwa kuzingatia maelekezo ya
Tume maalum iliyochunguza dosari zilizojitokeza kwenye matokeo ya mtihani wa
Kidato cha Sita mwaka 2012 katika somo la Islamic Knowledge.
3.2 Matokeo ya Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa
wa shule 159,609 kati ya watahiniwa 397,138
waliofanya Mtihani
wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana walikuwa ni 60,751 na
wavulana walikuwa ni 98,858.
3.3 Matokeo ya
Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa
wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 26,191 kati ya watahiniwa 61,001
waliofanya
mtihani. Wasichana
waliofaulu ni 11,581 na wavulana ni 14,910.
4.0
UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule
unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 35,349 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 10,924 na wavulana ni 24,425.
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule
mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Wavulana
|
Wasichana
|
Jumla
|
||||
Idadi
|
Asilimia
|
Idadi
|
Asilimia
|
Idadi
|
Asilimia
|
|
I
|
2,179
|
1.07
|
1,063
|
0.64
|
3,242
|
0.88
|
II
|
7,267
|
3.58
|
3,088
|
1.85
|
10,355
|
2.8
|
III
|
14,979
|
7.37
|
6,773
|
4.05
|
21,752
|
5.87
|
I-III
|
24,425
|
12.02
|
10,924
|
6.54
|
35,349
|
9.55
|
IV
|
74,433
|
36.65
|
49,827
|
29.78
|
124,260
|
33.54
|
I-IV
|
98,968
|
48.66
|
60,779
|
36.30
|
159,747
|
43.08
|
0
|
104,259
|
51.33
|
106,587
|
53.7
|
210,846
|
56.92
|
5.0
SHULE KUMI BORA NA SHULE KUMI ZA MWISHO
Ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo
cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 na F = 5. Shule zimegawanywa katika makundi mawili
kulingana na idadi ya watahiniwa kama ifuatavyo:
(i)
Shule zenye
watahiniwa 40 na zaidi (Jumla ni
3,396)
(ii)
Shule zenye
watahiniwa pungufu ya 40 (Jumla ni
753).
5.1 Shule Kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 40
na zaidi
Shule zifuatazo
zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi katika kundi la shule zenye
watahiniwa 40 na zaidi.
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI
|
MKOA
|
RANK
|
CENTRE NAME
|
REGISTERED
|
REGION
|
1
|
ST. FRANCIS GIRLS S S
|
90
|
MBEYA
|
2
|
MARIAN BOYS' S S
|
75
|
PWANI
|
3
|
FEZA BOYS' S S
|
69
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
MARIAN GIRLS S S
|
88
|
PWANI
|
5
|
CANOSSA S S
|
66
|
DAR ES SALAAM
|
6
|
FEZA GIRLS' S S
|
50
|
DAR ES SALAAM
|
7
|
ROSMINI S S
|
78
|
TANGA
|
8
|
ANWARITE GIRLS S S
|
49
|
KILIMANJARO
|
9
|
ST. MARY'S MAZINDE JUU S S
|
83
|
TANGA
|
10
|
JUDE MOSHONO SS
|
51
|
ARUSHA
|
5.2
Shule Kumi za mwisho zenye watahiniwa 40 na
zaidi
Shule zifuatazo
zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi kutoka mwisho.
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI
|
MKOA
|
1
|
MIBUYUNI S S
|
40
|
LINDI
|
2
|
MAMNDIMKONGO S S
|
63
|
PWANI
|
3
|
CHITEKETE S S
|
57
|
MTWARA
|
4
|
KIKALE S S
|
60
|
PWANI
|
5
|
ZIRAI S S
|
41
|
TANGA
|
6
|
MATANDA SECONDARY SCHOOL
|
53
|
LINDI
|
7
|
KWAMNDOLWA S S
|
89
|
TANGA
|
8
|
CHUNO S. S
|
143
|
MTWARA
|
9
|
MBEMBALEO S S
|
56
|
MTWARA
|
10
|
MAENDELEO S S
|
103
|
DAR ES SALAAM
|
5.3
Shule Kumi bora katika kundi la shule zenye
watahiniwa chini ya 40
Shule zifuatazo
zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi.
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI
|
MKOA
|
1
|
THOMAS MORE MACHRINA SS S
|
20
|
DAR ES SALAAM
|
2
|
QUEEN OF APOSTLES-USHIROMBO SEMINARY
|
24
|
SHINYANGA
|
3
|
BETHELSABS GIRLS S S
|
33
|
IRINGA
|
4
|
PRECIOUS BLOOD S S
|
34
|
ARUSHA
|
5
|
MAUA SEMINARY
|
31
|
KILIMANJARO
|
6
|
ST. MARY'S JUNIOR SEMINARY
|
28
|
PWANI
|
7
|
CARMEL S S
|
36
|
MOROGORO
|
8
|
SANU SEMINARY
|
37
|
MANYARA
|
9
|
BROOKEBOND S S
|
27
|
IRINGA
|
10
|
ST.CAROLUS SECONDARY
S S
|
37
|
SINGIDA
|
5.4
Shule kumi (10) za mwisho zenye watahiniwa
chini ya 40
Shule
zifuatazo zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi kutoka mwisho.
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI
|
MKOA
|
1
|
DODEANI TECH. S S
|
10
|
PEMBA
|
2
|
KALAMBA S S
|
11
|
DODOMA
|
3
|
HURUI S S
|
12
|
DODOMA
|
4
|
USUNGA S S
|
13
|
TABORA
|
5
|
MANDWANGA S S
|
13
|
LINDI
|
6
|
BETTY MITCHEL S S
|
17
|
MOROGORO
|
7
|
CHONGOLEANI S S
|
17
|
TANGA
|
8
|
MMULUNGA S S
|
17
|
MTWARA
|
9
|
NYUAT S S
|
20
|
ARUSHA
|
10
|
MWAKIJEMBE S S
|
13
|
TANGA
|
6.0. HITIMISHO
Kuanzia sasa matokeo ya mithani ya kidato cha Nne na
Sita yatachakatwa kwa kutumia Fixed Grade Range na Standardisation. Natoa wito
kwa wadau wote wa elimu kutoa ushirikiano tuweze kuboresha elimu nchini.
7.0.
KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)
2012
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE), 2012
yanapatikana katika tuvuti zifuatazo :
Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (Mb)
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
30/5/2013
No comments:
Post a Comment