JAMHURI
YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia
nafasi za kazi kwa wote wenye taaluma za Kada
za Afya ambao wako tayari kufanya kazi katika Utumishi wa Umma.
Vigezo na Masharti:
1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
3. Watumishi wa Kada za
Afya waliojiendeleza wakiwa kazini wasitume maombi bali waombe kwa Waajiri
wao kubadilishwa vyeo kulingana na sifa
walizopata.
4. Maombi yote yaambatanishwe: Nakala ya Cheti cha Taaluma, Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne/Sita,
Maelezo binafsi (CV), Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni, Nakala ya
cheti cha usajili au leseni ya kufanya kazi ya Taaluma husika.
5. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha Nne/Sita ni
lazima vithibitishwe na Hakimu au Wakili
anayetambuliwa na Serikali.
6. Waombaji wanatakiwa kuchagua/kupendekeza maeneo matatu
(Mikoa na Halmashauri) ambayo wangependa
kupangiwa kazi kwa kuzingatia nafasi zilizoainishwa kwenye Kibali (Tazama
Tovuti ya Wizara).
7. Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu, maombi yake hayatashughulikiwa.
8. Watumishi ambao walikwishapangiwa vituo vya kazi miaka ya nyuma na
hawakuripoti
au kuacha kazi hawatapangiwa vituo vya kazi, kwa sababu
hawataweza kuingia kwenye ‘Payroll’ ya
Serikali.
Waajiri wote wanatakiwa kuharakisha zoezi la kuwaajiri na kuwaingiza
kwenye ‘Payroll’ ya Serikali wataalam wote watakaopangiwa vituo vya kazi kwenye
mamlaka zao ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kujikimu kwa wakati ili
kuwaondolea usumbufu usio wa lazima watumishi husika.
Aidha, Waajiri wanakumbushwa kukagua na kuthibitisha uhalali wa vyeti vya kidato cha Nne na Sita vya
wataalam hao kwa kuviwasilisha Baraza la Mitihani la Taifa ili wale
watakaobainika kujipatia ajira kwa kutumia vyeti vya kughushi washitakiwe kwa
mujibu wa sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hatatoa
barua za kupangiwa Vituo vya kazi. Majina
ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz). Utatakiwa kuripoti
kwenye Kituo ulichopangiwa kazi ndani ya
siku 14 kuanzia tarehe ya toleo la
kupangiwa kazi kwenye tovuti ukiwa na vyeti vyako halisi (Original).
Maombi yote yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe
hayatafanyiwa kazi.
Barua
zote zitumwe kwa njia ya posta nafasi inayoombwa kupitia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 7 Februari,
2014.
Tangazo hili pamoja na mchanganuo wa nafasi za kazi vinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz)
No comments:
Post a Comment