Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Wanachi wa Tanzania, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange, akimkabidhi
hati ya kustaafu Jeshi, Luteni Jenerali
Sylvester Rioba mara baada ya sherehe ya kuwaaga Majenerali wastaafu katika
hafla iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Mgulani Jijini
Dar es Salaam Septemba 27, mwaka huu.(Picha na JWTZ)
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI
YA HABARI NA UHUSIANO
Simu
ya Upepo : “N G O M E”
Makao Makuu ya Jeshi,
Simu
ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex :
41051 DAR
ES SALAAM, 27 Septemba, 2013.
Tele
Fax :
2153426
Barua
pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa
Vyombo vya Habari
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange,
aliwaaga Maafisa wakuu waliostaafu rasmi kwa tarehe tofauti hadi Septemba 23,
mwaka 2013, baada ya kutimiza umri wao wa lazima wa kustaafu utumishi Jeshini.
Maafisa
hao waliagwa kwa gwaride rasmi ambalo lilifanyika katika Kambi ya Twalipo Mgulani
Jijini Dar es Salaam Septemba 27, mwaka
2013.
Maaflisa
wakuu hao ni pamoja na Luteni Jenerali Sylvester Rioba, Meja Jenerali Grace
Mwakipunda, Meja Jenerali Farrah Mohamed, Meja Jenerali Patric Mlowezi,
Brigedia Jenerali Stephen Ndazi, Brigedia Jenerali Daniel Matiku na Brigedia
Jenerali Lailo Chando.
Aidha, makamanda hao waliweza kushika nyadhifa
mbalimbali katika JWTZ wakati wa utumishi wao.
Luteni Jenerali Rioba mpaka anastaafu alikuwa
Mkurugenzi wa idara ya uratibu wa Maafa – Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali
Mwakipunda alikuwa mkuu wa tawi la Utumishi jeshini, Meja Jenerali Farrah
Mohamed alikuwa mkuu wa tawi Utendaji Vita na Mafunzo jeshini, Meja Jenerali
Mlowezi alikuwa mkuu wa tawi la ugavi na
uhandisi jeshini, Brigedia Jenerali
Ndazi alikuwa Kamishina msaidizi wa maendeleo Jeshini, Brigedia Jenelali Matiku
alikuwa Mkurugenzi wa miundo mbinu Jeshini na Brigedia Jenerali chando ambaye
alikuwa Mkurugenzi wa ustawi wa jamii Makao Makuu ya Jeshi la kujenga
Taifa(JKT).
Meja Jenerali Mwakipunda alikuwa ni Afisa wa
tatu mwanamke kuandishwa Jeshini baada ya Meja Jenerali mstaafu Zawadi Madawili
aliyestaafu Juni 30, 2008 ambaye alikuwa ni afisa wa kwanza mwanamke
kuandikishwa Jeshini na kanali mstaafu Easter Katemba ambaye alikuwa Afisa
mwanamke wa pili kuandikishwa Jeshini na alistaafu Juni 30, 2004.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment