Kaimu Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania(TET),
Dk, Leonard Akwilapo,(kushoto) akizungumza na waandishi Dar es Salaa kuhusu
Utekelezaji wa Majukumu mbalimbali ya Taasisi hiyo ikiwepo Ukuzaji wa Mitaala.Wengine
ni Mkurugenzi Idara ya Ubunifu na Uboreshaji Mitandao,Angela Katabaro na
Mkurugenzi Utafiti,Habari na Machapisho,Makoye Wangeleja.
Taasisi ya Elimu Tanzania
ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 13 ya Mwaka 1975. Hii ni Taasisi ya umma
iliyo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. TET imepitia mabadiliko
kadhaa ya kimfumo, ingawa kwa kiasi kikubwa bila kuathiri majukumu yake ya
msingi ambayo yameainishwa katika sehemu ya 2 ya taarifa hii. Kati ya mwaka
1965 – 1975 ilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa imeanzishwa na
Baraza la Chuo hicho na ilijulikana kama Taasisi ya Elimu. Mwaka 1975
taasisi ilitoka katika himaya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa taasisi
inayojitegemea. Mnamo mwaka 1987, taasisi ilibadilishwa jina na kuwa Taasisi
ya Ukuzaji Mitaala. Baadaye mwaka 1993 taasisi ilibadilishwa tena jina na
kuwa Taasisi ya Elimu Tanzania, jina hilo linaendelea kutumika hadi leo.
Sababu kubwa ya kubadilisha jina na ukweli kuwa taasisi inajihusisha na mambo
mengi ya kitaalamu zaidi ya ukuzaji mitaala. Hivyo ilionekana kuwa si sahihi
kuitambulisha kwa shughuli moja tu ya mitaala.
Kuanzia mwezi Julai 2009 TET
ilipandishwa hadhi kuwa Taasisi ya Elimu ya Juu isiyokuwa chuo kikuu kwa
kuzingatia jukumu lake la utoaji wa mafunzo ya kitaalamu yanayohitaji tuzo
mbalimbali. Hivyo, TET imesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(National Council for Technical Education/NACTE). Madadiliko haya yaliambatana
na jukumu la kuendesha mafunzo na kutoa tuzo TET; Taarifa
kwa Umma 2013 2
mbalimbali
zikiwemo za cheti, stashahada na shahada katika ubunifu na ukuzaji mitaala bila
kuathiri majukumu yake ya kisheria yaliyoainishwa katika Sheria anzilishi
iliyotajwa hapo juu.
2.0 MAJUKUMU YA TAASISI YA
ELIMU TANZANIA
2.1 Jukumu Kuu Jukumu kuu la TET ni kutafsiri kwa vitendo sera
mbalimbali za Serikali katika programmu za kielimu na mitaala inayowezesha
utoaji wa elimu bora kwa ngazi za elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya
ualimu. 2.2 Majukumu Mahususi Kwa mujibu wa Kifungu Na. 4 cha Sheria ya
TET Na. 13 ya Mwaka 1975, na kwa muhtasari chini ya taarifa hii, majukumu
mahususi ya Taasisi ya Elimu Tanzania yamo katika maeneo makuu manne yafuatayo:
(a) Ubunifu na Uboreshaji Mitaala Katika kutekeleza jukumu hili TET
hufanya yafuatayo:
(i) Kubuni
na kuandaa mitaala;
(ii) Kuboresha
na au kubadilisha mitaala*.
(iii)
Kuandaa, kurekebisha au kubadilisha
mihtasari ya masomo kwa kuzingatia mtaala ulioboreshwa.
* Ufafanuzi:
Ø “Mtaala”ni mwongozo wa utoaji elimu unaobainisha ujuzi, yaani
stadi, maarifa na mwelekeo wa kitabia unaokusudiwa kutolewa katika ngazi fulani
ya elimu, njia za kufundishia na kujifunzia, rasilimali mbalimbali
zinazohitajika katika kufundishia na
TET; Taarifa kwa Umma 2013 3
kujifunzia, utaratibu wa
kutathmini wanafunzi, muda wa mafunzo na tuzo za elimu zitakazotolewa.
Ø “Kuboresha mtaala” ni mchakato endelevu wa kufanya marekebisho madomadogo kwenye mihtasari
ya masomo bila kuathiri mtaala kwa jumla. Maboresho ya mtaala yanaweza kutokea
mara kwa mara kadri taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa
mitaala zinavyoweza kuonesha. Mfano:
Hatua ya kutenganisha somo
la Fizikia na Kemia kutoka somo moja na kuwa masomo mawili mwaka 2007 ni kitendo
cha kuboresha mtaala
Ø “Kubadilisha
mtaala” maana yake ni kufanya mageuzi
makubwa yanayoathiri mtaala. Mabadiliko ya mitaala hutokea kwa nadra hasa
kunapokuwa na mabadiliko makubwa katika mfumo wa Taifa wa kisiasa, kiuchumi,
kijamii na hata kiteknolojia.
Mfano: Azimio la Arusha la Mwaka 1967 lilibadilisha mfumo wa
kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hii ilfuatiwa na mabadiliko ya mitaala katika
nyakati tofauti yakiwemo mabadiliko ya mwaka 1979 ambapo masomo ya michepuo
(Kilimo, Ufundi, Sayansi Kimu na Biashara) yaliingizwa kwenye mitaala. Lengo
lilikuwa ni kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Elimu ya Kujitegemea iliyoasisiwa
katika Azimio hilo. (b) Uandaaji
wa Vifaa vya Kielimu Yafuatayo hufanyika:
(i) Kuandika na kuchapisha
vitabu vya kiada na ziada;
TET; Taarifa kwa Umma 2013 4
(ii)
Kuandaa vifaa mbalimbali vya kujifunzia na kufundishia kama vile vivunge vya
masomo (subject kits), miongozo, chati na vifaa vya elektroniki kwa mfano:
diski za video na za kusikiliza.
(iii)
Kubuni mbinu za kufaragua (improvise) visaidizi vya kufundishia (teaching aids)
kwa ajili ya kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji;
(iv) Kuweka viwango vya ubora
wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
(c) Utoaji Mafunzo ya
Mitaala Mafunzo kwa walimu, wakaguzi
wa shule, maafisa mitihani, maafisa elimu na wadau wengine wahusikao na
utekelezaji au usimamiaji wa elimu hutolewa katika maeneo makuu yafuatayo:
(i)
Mafunzo kabilishi kuhusu maboresho/mabadiliko ya mitaala;
(ii)
Mbinu bora za ufundishaji na ujifunzaji;
(iii) Mafunzo ya muda mrefu
kuhusu ubunifu na utekelezaji wa mitaala (kwa sasa TET inaendesha programu ya
Stashahada ya Uzamili Katika Ubunifu na Ukuzaji Mitaala).
(d) Utafiti na Ushauri wa
Kitaalamu Chini ya jukumu hili TET
hutekeleza yafuatayo:
(i)
Kufanya utafiti kuhusu masuala/matatizo mbalimbali ya kielimu;
(ii)
Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mitaala;
(iii)
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali na wadau wengine wa elimu au kuchukua
hatua zilizo ndani ya mamlaka ya TET kwa lengo la kuinua ubora wa elimu kwa
kuzingatia taarifa za utafiti.
(iv) Kuelimisha wadau na umma
kwa jumla kuhusu masuala ya elimu.
TET; Taarifa kwa Umma 2013 5
3.0 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
YA TET
3.1 Miongozo ya Utekelezaji
wa Majukumu ya TET Katika kutekeleza
majukumu yake yaliyoainishwa hapo juu, TET huzingatia miongozo ifuatayo:
(a)
Sheria ya TET Na. 13 ya Mwaka 1975;
(b)
Sera, mipango, maelekezo na vipaumbele vya Serikali kupitia nyaraka na matamko
mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
(c) Mpango Mkakati wa TET wa
Miaka Mitano (uliopo ni wa mwaka 2011 – 2016).
3.2 Utekelezaji wa Majukumu
ya TET Katika Kipindi cha Miaka Mitatu Iliyopita (2009/2010 Hadi 2011/2012)
Katika kipindi hicho kazi
zilizotekelezwa kwa kuzingatia mipango ya kazi ya kila mwaka zipo katika maeneo
makuu matatu yafuatayo:
(a) Uandaaji wa Mihtasari na
Miongozo ya Masomo
Kazi zifuatazo zilitekelezwa:
(i) Kuboresha mihtasari ya
masomo 26 ya ualimu ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi;
(ii) Kuboresha mihtasari ya
masomo 28 kwa masomo ya ualimu ngazi ya stashahada.
(iii) Kwa kushirikiana na Ofisi
ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, TET ilichapisha na kusambaza mihtasari na miongozo ya
masomo yote ya shule za msingi. Ambapo:
TET; Taarifa kwa Umma 2013 6
Jumla
ya mihtasari 30,908 ilisambazwa katika mikoa 21 ya Tanzania Bara na kila shule
ilipata nakala 2.
Mihtasari 105 iligawiwa kwa Waratibu wa Elimu nakala tano (5) kwa kila mmoja.
Jumla ya miongozo 15,424
ilisambazwa katika mikoa 21 na kila shule ilipata nakala moja.
(iv) Kuboresha mihtasari 25 ya
kufundishia masomo ya sekondari kidato cha V na VI.
(v) Kuchapisha mihtasari ya
masomo 25 ya kidato cha V na VI.
(vi) Kuandika mihtasari miwili
(2) ya somo la Ujasiriamali kwa shule za sekondari na vyuo vya ualimu ngazi ya
Stashahada.
(vii)
Kuandaa jumla ya mihtasari 36 ya Elimu Maalum kwa mafunzo ya ualimu katika
mchanganuo ufuatao:
Mihtasari 19 ya ngazi ya stashahada; na
Mihtasari 17 ya ngazi ya
cheti.
(viii) Kuchapisha Moduli 9 za
masomo ya ualimu ngazi ya stashahada na 14 ngazi ya Cheti.
(ix) Kuboresha na kuchapisha
miongozo 18 ya kufundishia masomo ya sekondari kidato cha I-IV.
(x) Kuchapisha na kusambaza
maandiko sita (6) ya mitaala (Curriculum Documents) kwa shule na vyuo vya
ualimu.
TET; Taarifa kwa Umma 2013 7
Uendeshaji wa Mafunzo ya Mitaala
Kazi zilizotekelezwa ni kama
ifuatavyo:
(i) Kuendesha mafunzo kwa walimu
wa shule za msingi wapatao 510 wa masomo ya Hisabati, Kiingereza na Sayansi
katika jumla ya Wilaya/ Halmashauri 17.
(ii) Kuendesha mafunzo kwa
walimu 240 katika wilaya za Masasi, Tunduru, Same, Kishapu, Meatu, Musoma (V),
Ukerewe, Bariadi na Bunda kuhusu mtaala wa elimu ya msingi uliboreshwa.
(iii) Kuendesha mafunzo juu ya
utekelezaji wa mtaala wa sekondari ulioboreshwa kwa walimu 30 wa shule za
sekondari Mazinde Juu.
(iv) Kuendesha mafunzo kwa
walimu 45 na Afisa Elimu Taaluma na Mkaguzi wa Shule za Sekondari za wilaya ya
Pangani.
(v) Kuendesha mafunzo ya
ufundishaji bainifu (diagnostic teaching kwa wakufunzi 34 wa vyuo vya ualimu
ngazi ya cheti.
(vi) Kuendesha mafunzo ya
mitaala (competence –based curriculum) kwa Waratibu wa Mitaala 50 na wataalamu
36 kutoka nchi 8 za Afrika kupitia programu za Elimu ya Msingi Katika Afrika
(Basic Education in Africa Programmes/ BEAP) kwa kushirikiana na UNESCO.
TET; Taarifa kwa Umma 2013 8
(vii) Kuendesha mafunzo kwa
walimu 200 wa somo la French kwa shule za sekondari katika kanda zote 11 za
elimu Tanzania Bara.
(viii) Kuendesha mafunzo kwa
wakufunzi 64 wa vyuo 16 vya ualimu ngazi ya stashahada.
(ix) Kuendesha mafunzo ya
Programu ya Stashahada ya Uzamili katika Ubunifu na Ukuzaji Mitaala
(Postgraduate Diploma in Curriculum Design and Development - PGDCDD). Programu
hii imekuwa ikipata wanafunzi kutoka takribam mabara yote ya dunia na imekuwa
na mafanikio kama ifuatavyo:
§ Awamu
ya kwanza: Oktoba 2011; waliodahiliwa 49 na waliofaulu 42 (85.7%).
§ Awamu
ya pili: Novemba 2012; waliodahiliwa 47, waliofaulu 43 (91.5%).
§ Awamu
ya tatu: Desemba 2013; waliodahiliwa ni 75, na mafunzo yanaendelea.
Tanbihi (N. B.): Mafunzo haya yanalenga kuwa na wataalamu wengi
waliobobea katika fani ya ukuzaji na utekelezaji wa mitaala ili kuinua ubora wa
elimu na kuchochea kasi ya maendeleo. Kwa wastani Watanzania 20 wamekuwa
wakipata mafunzo haya kila mwaka na kuna uwezekano mkubwa wa idadi hii
kuongezeka kadri siku zinavyokwenda. TET; Taarifa kwa
Umma 2013 9
Kabla
ya mwaka 2011 fani ya ukuzaji na ubunifu wa mitaala imekuwa haitolewi na chuo
chochote hapa nchini kama eneo la utaalamu linalojitegemea bali kama sehemu tu
ya kozi nyingine. Tunatumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati UNESCO na Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania kwa kushirikiana nasi katika kuendesha programuu hii
kila mwaka. Tunaishukuru pia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ambayo ilihakiki
na kuidhinisha mtaala wa programu hiyo. (c) Ufuatiliaji na Tathmini ya
Mitaala Kazi zifuatazo zilitekelezwa:
(i) Kuanzisha na kutekeleza
Mpango wa Ushirikiano kati ya TET na shule (TIE-School Partnership) ambao
unahusu Waratibu wa Mitaala kuwa na vipindi maalumu vya kufanya kazi shuleni
kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mitaala na kubaini
changamoto zilizopo kwa lengo la kuzifanyia kazi. Kwa kuanzia mpango huu
unatekelezwa katika shule za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
(ii) Kufanya ufuatiliaji wa
utekelezaji wa mitaala katika ngazi mbalimbali hivyo kuwezesha kupata taarifa
zilizotumika kuboresha mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu
kama ilivyoelekezwa hapo juu.
4.0 CHANGAMOTO
Changamoto kuu katika
kutekeleza kazi za kitaaluma zinajumuisha upungufu/ukosefu wa tengo la fedha
kwa ajili ya shughuli za mitaala TET; Taarifa kwa
Umma 2013 10
na
upungufu wa vitendea kazi hususan vifaa vya ofisi kama kompyuta. Tatizo hili
limekuwa likishughulikiwa kwa kutafuta vyanzo mbadala vya fedha kama vile
kushirikiana na wadau wa elimu na kutumia vyanzo vya ndani vya mapato. Baadhi
wa wadau wakuu wanaoshirikiana na TET katika kuendesha miradi ya kielimu ni
UNESCO, NUFFIC, USAID, UNICEF, Wizara ya Ujenzi (kuhusu Elimu ya Usalama
Barabarani) na Wizara ya Afya (elimu ya VVU na UKIMWI) – kwa kutaja wachache.
Tunatumia fursa hii kuwashukuru sana wadau hawa wa elimu na wengine wengi ambao
hatujawataja.
5.0 MIPANGO YA BAADAYE
Kwa kuzingatia Mpango Mkakati
wa TET wa Maendeleo ya Miaka Miatano (2011- 2016), TET inakusudia
kufanya yafuatayo katika kipindi hicho:
(i)
Kufanya tahakiki (review) ya mitaala katika ngazi zote.
(ii)
Kuandaa vifaa vya kujifunzia na kufundishia vikiwemo vitabu, vifaa vya
kielektroniki na na programu za redio na runinga;
(iii)
Kukamilisha andiko la Mwongozo wa Taifa wa Ukuzaji Mitaala;
(iv)
Kufanya tathmini ya utekelezaji wa mitaala ya elimu ya awali, msingi na
sekondari;
(v) Kuendesha makongamano ya
kitaifa na kimataifa kuhusu mitaala;
TET; Taarifa kwa Umma 2013 11
(vi) Kujenga kituo cha kisasa
cha mafunzo ya ukuzaji mitaala katika kiwanja cha TET Mikocheni;
(vii) Kuendesha mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa kiutendaji Waratibu wa Mitaala wa TET;
(viii) Kuandika na kutekeleza
sera ya utafiti na uelekezi wa kitaalamu;
(ix) Kuendesha mafunzo elekezi
kwa walimu na watekelezaji wengine wa mitaala kuhusu utekelezaji wa mitaala.
6.0 HITIMISHO
Nawaomba
Watanzania wote, washirika wa maendeleo hasa katika sekta ya elimu na wadau
wote wa elimu wakiwemo wa sekta binafsi, kushirikiana na TET katika juhudi za
kutoa elimu iliyo bora kwa watoto na umma wa Watanzania. Wanaweza kuwasiliana
nasi kupitia tovuti ta TET ambayo ni www.tie.go.tz. Tunakaribisha maswali,
hoja, mipango ya kuboresha elimu na hata ukosoaji wa kujenga ili tuendelee
kuboresha elimu kwa manufaa ya watu wetu na nchi yetu. Mwisho naishukuru sana
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kutupatia fursa hii adhimu
ya kuwasiliana na Watanzania. Na vile vile tunatoa shukrani nyingi kwenu
waandishi wa habari kwa kuhudhuria kongamano hili; tunatarajia kuwa mtafikisha
taarifa hizi kwa wananchi. ASANTENI SANA Dkt. Leonard D. Akwilapo Kaimu
Mkurugenzi Mkuu TAASISI YA ELIMU TANZANIA
No comments:
Post a Comment