KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, November 30, 2017

WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG.


 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF),  Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo wakati viongozi wa Mfuko walipokuwa wakiwasilisha taarifa za utendaji wake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, jijini Arusha.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipinmdi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.

Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili nay a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha.
Amesema Mfuko umekuwa ukiaandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uaandaji wa hesabu za fedha na kwa mujibu wa sheria CAG ndiye mwenye mamlaka ya kufanya ukaguzi na Hati Safi ni uthibitisho wa taarifa ya fedha za Mfuko kuonyesha hali halisi na kutokuwa na dosari ya aina yoyote.
Amesema katika ukaguzi huo, CAG alishirikiana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC). Mwakilishi wa kutoka Ofisi ya CAG,  amethibitishia wajumbe usahihi wa taarifa hiyo ya fedha ya WCF.
Mkutanmo huo ambao  umebeba kauli mbiu isemayo, "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, pia ulipokea taarifa ya mipango ya uwekezaji ambapo.  Kwala aliwaambia wajumbe kuwa, katika kipindi kati ya mwaka 2017/18 – 2021/22, Mfuko umepanga kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayoleta faida kwa mujibu wa tathmimi za kitaalamu zitakazofanyika.
“Maeneo tuliyoyaanisha katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda ni pamoja na kiwanda cha Grape Processing Factory kwa ushirikiano kati ya  GEPF na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, kiwanda cha Madawa mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Kiwanda cha Morogoro Canvas Mills kwa kushirikiana na mifuko ya WCF, NSSF, PSPF, GEPF, na LAPF”. Alifafanua.
Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa Mfuko kuwekeza, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba alisema, fedha zitokanazo na michango ya Wanachama ni kidogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya ulipaji Mafao ya fidia na kwa hali hiyo, ni muhimu Mfuko kuwekeza ili kupanua wigo wa kuongeza mapato na hivyo kuendelea kutoa Mafao ya Fidia bila ya shaka yoyote.
 Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa WCF wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, akizungumza
 Mkurugenzi wa Fedha wa WCF, Bezil Kwala, akiwasilisha ripoti ya fedha ya Mfuko kwa mwaka wa 2015-2016.
 Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Ofisi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Johanes Joel Kisiri, akisikiliza uwasilishaji wa taarifa hiyo ya fedha.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha WCF, Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria juu ya kuanzishwa kwa Mfuko na jinsi unavyofanya kazi zake. Pamoja na mambo mengine Siyovelwa aliwaambia wajumbe kuwa,   Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoazishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura Na. 263 (Marejeo ya 2015) na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015. Lengo la kuazishwa kwa Mfuko ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta rasmi (Binafsi na Umma) Tanzania bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Anslem Peter, akiwasilisha taarifa ya uendeshaji ya Mfuko katika kipindi cha uahai wake, ambapo alisema Mfuko umekuwa ukifanya vizuri ikiwa ni pamoja na usajili wa wanachama " katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015-2017 jumla ya Waajiri 5,178 walisajiliwa ikiwa ni asilimia 71.92 ya lengo la kusajili waajiri 7,200
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dk.Irene Isaka.
 Kiongozi wa chama cha Waajiri nchini (ATE), Aggrey Mlimuka, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Hiroshi Yamabana kutoka Shirika mla Kazi Duniani, (ILO), akiuliza masuala mbalimbali kuhusu upembuzi juu ya usalama mahala pa kazi
 Tommie Dounball, kutoka kampuni ya Argen ya Afrika Kusini, akizungumzia uzoefu wa masuala ya Mfuko wa Fidia kutoka nchini kwake

 Mshomba (kushoto), akizungumza jambo wakati wa mkutano huo. Kulia ni Tommie Dounball, kutoka kampuni ya Argen ya Afrika Kusini,

 Mbunge wa jimbo la Mlalo Mkoani Tanga, Rashiud Shangazi, (kushoto), akimsikiliza Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele. Wote hao ni miongoni mwa wadau walioalikwa kushiriki mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wdhamini ya WCF, Emmanuel Humba, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Taifa wa Bima ya Afya, (MHIF), Afya, Bernard Konga.
Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),  Lightness Mauki

Wednesday, November 29, 2017

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA HUDUMA MPYA YA WCF YA WAAJIRI KUJISAJILI KWENYE MTANDAO WA INTERNET.

Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Stephen Goyayi, akielezea jinsi huduma hiyo iyakavyofanya kazi.
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID. ARUSHA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amezindua huduma mpya itakayowawezesha waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kutumia mtandao wa Internet.
Mhe. Mhagama amezindua huduma hiyo wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, Arusha.
“Huduma hii itawawezesha waajiri kujisajili na Mfuko kupitia mtandao wa internet na hawalazimiki kujaza fomu na kuja ofisini kwetu au kwa maafuisa kazi” Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, alisema wakati akitambulisha huduma hiyo kwa Mhe. Waziri.
Katika hatua nyingine, Benki ya NMB Bank plc  imenyakua tuzo baada ya kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi.
Kampuni zingine zilizonyakua tuzo kundi la waajiri ni Steel Master Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji nyaraka za madai ya fidia kwa wafanyakazi na kampuni nyingine ni KPMG  Advisory Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michango miongoni mwa kundi la waajiri wenye wafanyakazi wengi.
WCF iliwatunukia tuzo wadau wa Mfuko huo ambapo Waziri Jenista kwa niaba ya Serikali alipokea tuzo hiyo, kwa kutambua mchango wa Serikali katika kuanzisha na kufanikisha utendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Wadau wengine ni Shirika la Vyama vya Wafanyakazi, (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), kwa kutambua ushiriki wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshjomba, wakishuhudia Mwenyekiyti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilinhi milioni 15, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, ikiwa ni mchango wa Mfuko kusaidia mpango wa elimu mkoani humo. Makabidhiano haya yamekwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa WCF jijini Arusha
 Waziri Mhagama (watatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Eric Shitindi, (wakwanza kushoro), wakipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioini 33.8 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, (wapili kushoto). Fedhab hizo ni kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa komputa nundu (perkins Braille Machines) kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona katika shule za umma.
 
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya WCF,. Wakwanza kushoto ni katibu wa Waziri Jenista Mhagama.
 Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Richard L.Makungwa kutoka NMB Bank Plc tuzo ya mwajiri mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba.
 Mheshimiwa Waziri akimkabidhi tuzo Kaimu Mwenyekiti wa ATE, Janet Reuben Lekashingo tuzo ya ushiriki kama Mdau wa WCF. Anayeshuhudia ni Humba.
Mheshimiwa Waziri akimkabidhoi tuzo Kaimu Mwenyekiti wa ATE, Tumaini Peter Nyamhokya, Katibu Mkuu wa TUCTA, tuzo ya ushiriki kama mdau wa WCF. Anayeshuhudia ni Humba.
 Mheshimiwa Mhagama akimkabidhi tuzo, Hiroshi Yamobana kutoka ILO kwa ushiriki na kama mdau
 Waziri Jensita akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba
 Mwenyekiti wa Boadi ya Wadhamini ya SSRA hadi Aprili 2017, Juma Muhimbi, (kulia), akiteta jambo na Masha Mshomba
 Waziri akipokea na Feddy Maro, wa AICC alipowasili mapema kufungua mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akizungumza
 Kamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, na Mbunge wa Chemba,  Juma Nkamia
 Sara Kibonde Msika kutoka SSRA
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dk, Irine Isaka akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF,  Adam Mayingu, wakati wa mkutano Mkuu wa Kwanza wa mwaka wa Wadau wa WCF.
Mmoja wa watu wanaofaidika na Mafao ya WCF.

TANESCO: HITILAFU KWENYE GRIDI YA TAIFA ASUBUHI HII.

MAJIRA ya saa 7:20 leo hii Alhamisi Novemba 30, imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha umeme kukatika takriban kwenye mikoa yote iliyounganishwa kwenye Gridi hiyo.


Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, mafundi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameanza kufuatilia kujua chanzo chake hasa ni nini na taarifa Zaidi zitatolewa kila baada ya muda ili kuufahamisha umma na watuamiaji wa umeme.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA WCF KWA KUPIGA HATUA KUBWA NDANI YA KIPINDI KIFUPI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Umlemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumnbi wa Simba, Kituo cga Mikutano cha Kimataifa, AICC Arusha.

  
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa mafanikio ambayo Mfuko umepayata katika kipindi cha muda mfupi tangu uanzishwe.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) jijini Arusha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema, katika kipindi kifupi cha miaka miwili tangu WCF ianizshwe Mfuko umeweza kutekeleza wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama na kulipa Mafao ya Fidia.
“Mfuko umeanza kufikia wanyonge kwani umeonyesha jinsi ambavyo wafanyakazi wanyonge waliokuwa hawalipwa fidia wanapopata madhara kazini, sasa kutokana na kuwepo kwa Mfuko huu wanyonge wameanza kufaidi matunda kama ambavyo serikali ilidhamiria.
“Nitoe wito kwa viongozi wa Mfuko, endeleeni kutoa elimu kwa wananchi hususan waajiri ili waweze kujisajili na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuwalipa fidia wafanyakazi wao pindi wanapopata madhara wawapo kazini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba amesema hali ya Mfuko ni njema tangu uanzishwe, “Tunapokutana leo hii kwa mara ya kwanza kabisa, napenda kuwajulisha kuwa Mfuko umekuwa ukifanya vizuri katika kuimarika kifedha ambapo kwa mwaka wa kwanza tu, Mfuko ulifikia kiasi cha shilingi Bilioni 65.68 na katika mwaka wake wa pili ambapo ndio huu tulio nao napenda kuwafahamisha kuwa Mfuko umekuwa hadi kufikia Shilingi Bilioni 135 fedha ambazo bado hazijakaguliwa lakini sitarajii tofauti kubwa sana hata zoezi la ukaguzi litakapofanyika”. Amesema, Mshomba.

Aidha, Mshomba alisema, madhumuni ya Mkutano huu wa siku mbili ambao umebeba kauli mbiu ya "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”.  ni kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko, kutathmini maendeleo na changamoto zinazoukabili Mfuko na kupokea maoni ya kuboresha huduma za Mfuko.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF,  Emmanuel Humba amesema, tangu Mfuko uanzishwe, umetoa mafunzo mbalimbali  kwa wadau wa Mfuko ikiwa ni pamoja na Madaktari.
“Hadi sasa Mfuko umetoa mafunzo kwa Madaktari 504 nchi nzima kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini za ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi”. Amesema, Humba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofiosi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mashomba, akitoa hotuba yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, akipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, wakati alipowasili kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, wakati akiwasili kqwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC jijini Arusha.
 Mhagama na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na 
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dk. Abdulsalaam Omar,

 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Anslem Peter.
 Afisa wa WCF, Edward Kirenga, (kushoto), akiwasajili wajumbe wa mkutano
 Kutoka kushoto, Waziri Mhagama, Dk, Irine Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Eric Shitindi na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, akitoa hotuba yake.

Dk, Isaka, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Stella Ikupa, (kushoto), wakati wa mkutano huo.
Kikundi cha bendi ya Mjomba, (Mrisho Mpoto), kikitumbuiza
Viongozi wakishuhudia burudani ya kikundi cha bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto.
Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Anselim Peter, (wapili kulia), akijadiliana jambo na maafisa wa Mfuko huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dk. Irine Isaka, (kulia), akisalimiana na Meneja Mafao wa WCF, Rehema Kabongo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshac Bandawe , (kushoto), akisalim iana na Meneje Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele.
Wajumbe wamkien delea kusajiliwa kabla ya kuingia ukumbini.
Mwenyekiti wa Bodi, Emmnuel Humba, (kulia), akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake wa bodi, Dk, Francis Michael, (wapili kulia), na Richard Wambali
Baadhi ya wakurugenzi nna mameneja wa WCF.