KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, September 27, 2013

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI YA WANANCHI YA WANANCHI WA TANZANIA ,JENERALI DAVIS ADOLF MWAMUNYANGEA,AWAAGA MAAFISA WAKUU WASTAAFU.



Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Wanachi wa Tanzania, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange, akimkabidhi hati ya kustaafu Jeshi, Luteni Jenerali Sylvester Rioba mara baada ya sherehe ya kuwaaga Majenerali wastaafu katika hafla iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Mgulani   Jijini     Dar es Salaam Septemba 27, mwaka huu.(Picha na JWTZ)



JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E              Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo  : DSM  22150463           Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                          DAR ES SALAAM,  27 Septemba, 2013.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe         : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                   : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
         
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange, aliwaaga Maafisa wakuu waliostaafu rasmi kwa tarehe tofauti hadi Septemba 23, mwaka 2013, baada ya kutimiza umri wao wa lazima wa kustaafu utumishi Jeshini.
Maafisa hao waliagwa kwa gwaride rasmi ambalo lilifanyika katika Kambi ya Twalipo Mgulani Jijini Dar es Salaam Septemba 27, mwaka  2013.
Maaflisa wakuu hao ni pamoja na Luteni Jenerali Sylvester Rioba, Meja Jenerali Grace Mwakipunda, Meja Jenerali Farrah Mohamed, Meja Jenerali Patric Mlowezi, Brigedia Jenerali Stephen Ndazi, Brigedia Jenerali Daniel Matiku na Brigedia Jenerali Lailo Chando.
Aidha, makamanda hao waliweza kushika nyadhifa mbalimbali katika JWTZ wakati wa utumishi wao.
Luteni Jenerali Rioba mpaka anastaafu alikuwa Mkurugenzi wa idara ya uratibu wa Maafa – Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Mwakipunda alikuwa mkuu wa tawi la Utumishi jeshini, Meja Jenerali Farrah Mohamed alikuwa mkuu wa tawi Utendaji Vita na Mafunzo jeshini, Meja Jenerali Mlowezi alikuwa mkuu wa tawi la  ugavi na uhandisi jeshini,  Brigedia Jenerali Ndazi alikuwa Kamishina msaidizi wa maendeleo Jeshini, Brigedia Jenelali Matiku alikuwa Mkurugenzi wa miundo mbinu Jeshini na Brigedia Jenerali chando ambaye alikuwa Mkurugenzi wa ustawi wa jamii Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa(JKT).


Meja Jenerali Mwakipunda alikuwa ni Afisa wa tatu mwanamke kuandishwa Jeshini baada ya Meja Jenerali mstaafu Zawadi Madawili aliyestaafu Juni 30, 2008 ambaye alikuwa ni afisa wa kwanza mwanamke kuandikishwa Jeshini na kanali mstaafu Easter Katemba ambaye alikuwa Afisa mwanamke wa pili kuandikishwa Jeshini na alistaafu Juni 30, 2004.

           

   
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.

No comments: