KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Monday, January 28, 2013

MSANII ELIZABETH MICHAEL 'LULU" APATA DHAMANA LAKINI VIGEZO HAVIKUKIDHI AKARUDISHWA RUMANDE.


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuachia kwa dhamana msanii wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael "Lulu" anayekabiliwa na mashitaka ya kuua bila kukusudia msanii Steven Kanumba,



Lulu aliwasilisha maombi ya dhamana kupitia kwa jopo la mawakili wake, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe, kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika.
Maombi hayo yaliwasilishwa chini ya hati ya dharura, wakitaka yasikilizwa na kuamriwa mapema kwa madai kuwa mshitakiwa amekaa rumande kwa muda mrefu.
Akisoma uamuzi huo jana Jaji Zainab Mruke alisema kuwa, mahakama imekubali ombi hilo la dhamana kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika na dhamana ni haki yake ya msingi.
 Lulu akifunika sura ndani ya Mahakama Kuu Dar es Salaam.

 Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa Lulu wakiwa Mahakama Kuu.
 Lulu akifunika sura huku akicheka ndani ya Mahakama Mkuu.
 Lulu akiwa ameshika tama ndani ya Mahakama Kuu Dar es Salaam.
 Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliofika Mahakama Kuu kufuatilia kesi ya Lulu.
.
 Lulu akicheka baada ya kuwaona ndugu jamaa na marafiki ndani ya Mahakama Kuu Dar es Salaam.
 Lulu akiomba mbele ya Askari Magereza Mahakama Kuu Dar es Salaam kabla ya hakimu kufika.
 Lulu akiwa na mawazo ya kutoka nje kwa dhamana na huku akiwa chini ya Ulunzi wa Askari Magereza.
 Askari Magereza wakimlinda Lulu baada ya kupatiwa dhamana Mahakama Kuu.
 Wakili wa Lulu,Peter Kabatala (mwenye suti) akizungumza na waandishi nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam.
 Waandishi wapigapicha wa Vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa nje ya Mahakama Kuu wakimsubiri Lulu kumpigapicha.

 Askari magereza wakimsindikiza Lulu kupanda gari na kurudi Gerezani.
 Lulu akiwa nje ya Mahakama Kuu ya Dar es Salaam akielekea kupanda gari la Magereza.
Lulu akipanda gari la Askari Magereza kuelekea rumande.

No comments: