KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Monday, March 27, 2017

PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango  wa PPF kwenye Jamii.

Saturday, March 25, 2017

MAKAMANDA WA POLISI KUKUTANA DODOMA KUPANGA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UHALIFU.


Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

MAOFISA Wakuu wa Jeshi la Polisi  wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi,  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba (pichani) alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao mkauu ya Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na Makamanda wa vikosi bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka 2017.

Aidha, Bulimba alisema mbali na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu kukabiliana na wahalifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika hapa nchini.
“Katika kikao hicho Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa,  mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini” Alisema Bulimba.

Bulimba alisema kikao kazi hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba ambapo kauli mbiu katika kikao hicho ni “Zingatia maadili tunapopambana na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya Taifa”.

KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AWAONDOA HOFU WANACHAMA WA PPF KUFUATIA UAMUZI WAKE WA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 26 wa Wamachama na Wadau wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), jijini humo Machi 24, 2017. Kauli mbiu ya Mkutano huo ilikuwa, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”.
Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Waziri alisema"Naomba niwatoe hofu Wanachama wa PPF, kuhusu uamuzi wa Mfuko kuwekeza kwenye viwanda, kwani uamuzi huu ni sahihi kwa sasa, ikizingatiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda, lakini pia Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kujenga uchumi wa viwanda." Alitoa hakikisho Waziri Mhagama.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw.William Erio, akionyesha furaha yake kufuatia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika mkutano huo ambapo alisema, jumla ya washiriki 800 walihudhuria mkutano huo na hivyo Mfuko umefanikiwa kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa, akizungumza kwenye mkutano huo. Yeye alisema Jeshi la Magereza limeamua kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo PPF na NSSF katika kutekeleza mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na PPF, wanafanya uwekezaji mkubwa katika kiwanda cha viatu kule gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro na kwenye kiwanda cha sukari kwenye shamba la Mbigiri mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, akifuatilia kwa makini mkutano huo

Friday, March 24, 2017

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea Mradi wa Umeme wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2017


Meneja Msimamizi wa Mradi wa Kinyerezi I, Yuka Mukaibo kutoka kampuni inayojenga mradi huo ya Sumitomo kutoka Japan, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati walipotembelea eneo la Mradi jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Palangyo, na wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James, (aliyesimama), akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliotembelea kujionea maendeleo ya Mradi huo