KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, September 25, 2013

TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO.

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
 
NAIBU  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala  amesma Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta ajira vijana pindi watakapokuwa tayari kuienzi kwa vitendo na kuisomea.
 
Makala alisema hayo mjini hapa alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tamasha la 32,  la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lenye kauli mbiu ‘Sanaa na Utamaduni katika kukuza utalii’ linaloshirikisha vikundi zaidi ya 70, kutoka ndani na nje ya Tanzania.
 
Akihutubia, umati wa wananchi,wanafunzi wa chuo hicho cha sanaa na vikundi mbalimbali vinavyoshiriki, Waaziri Makala alisema akiwa waziri mwenye dhamana atahakikisha utamaduni na sanaa nchini inakua huku ikiwanufaisha watu wote kwa vizazi vya sasa  na vya baadae.
 
“Katika kuenzi  Sanaa na Utamaduni, Wizara ina mipangilio mingi ikiwemo nay a kuakikisha tunakuza utamaduni wa Taifa letu na hata ajira kwa vijana ambao watajiunga na sanaa hivyo tutaendelea kushirikiana na chuo cha TasuBa  na wadau wengine katika kufikia malengo” alisema Makala.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Michael Kadinde  alisema  watahakikisha tamasha hilo kongwe nchini  wanafikia vikundi na wasanii  mbalimbali ilikupata kushiriki na kuonesha kazi zao.
 
“Lengo kufikia wasanii wote na hilo tunafanya kila mwaka na zaidi milango ipo wazi kwa mashirika binafsi ya ndani na nje kuja kuwekeza na kukuza sanaa zetu” alisema Kadinde
 
Na kuongeza kuwa kwa sasa TaSUBa ina enzi na kulithisha sanaa na utamaduni kwa vitendo ikiwemo kutoa mafunzo kwa watoto wadogo na wale wa elimu ya msingi.
 
..
Kwa upande wa Vikundi   vinavyoshiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na ;
Alisema, vikundi 40 kati ya 60, ni kutoka Tanzania na vingine ni kutoka nje ya nchi vikiwemo vilivyowahi kushiriki tamasha hilo na vipya ambavyo itakuwa ni mara ya kwanza kuja.
 
Alivitaja vikundi vya Tanzania kuwa ni Ngome International Magic Show – JWTZ,  Splendid Theatre, Kigamboni Community Centre, Malezi Youth Theatre na Jivunie Tanzania Sanaa.
 
Vingine ni Mapoloni Culture Centre, Albino Revolutionary, Cocodo African Music, Imani Theatre, Safi Theatre, Imara Boma, Bagamoyo House of Talents, Bwagamoyo Africulture, Godykaozya & Tongwa Band na Mtoto Mchoraji.
 
Vimo pia Shada Acrobatics, Bagamoyo Players, Bayoice, Jikhoman & Afrika Sana Band, Vitalis Maembe & The Spirit Band na Bagamoyo Dance Company.
 
Aidha, kuna vikundi vya Makini Organization (Arusha), Tumaini Group (Manyara), Kimanzichana Vijana Group (Mkuranga), Utandawazi Theatre Group (Matwi Gha Chalo), kutoka visiwa vya Ukerewe, Hiari ya Moyo (Dodoma), Moshi Police Academy (Moshi), CBM Acrobatic Group, Man Kifimbo Band na Midundo ya Sanaa. Pia kuna vikundi kutoka Ethiopia , Kenya , Norway , Uganda , Rwanda na Ujerumani.
 

No comments: