Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012 akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao 15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo, lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mkoani Mara
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012 wakiwa nje ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu akishuhudia kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao 15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo, lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mkoani Mara.
Mbwa mwitu wakirejea mbugani baada ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao 15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo, lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mkoani Mara.
Wahifadhi wakifungua wigo wa senyenge ili kuachia huru kundi la pili la mbwa mwitu 15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma hilo maalumu la Mradi huo, lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mkoani Mara
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Joseph Kaboya, mhifadhi wa boma maalumu la mradi huo katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mkoani Mara, kwa kufanikisha zoezi hilo kwa mara ya pili. Kushoto ni Meneja wa Mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wasimamizi na wafadhili wa Mradi huo.
No comments:
Post a Comment