Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 24
kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12 mwaka huu kuajianda kwa mechi
ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.
Katika
kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi
Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa
Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na
mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.
Pia
kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar
(Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe
la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji
hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.
Kikosi
kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na
Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni
(Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu
(Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa
Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).
Viungo
ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa
(Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum
Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).
ZAMBIA YATAJA KIKOSI CHA KUIVAA STARS
Kocha
Mkuu wa timu ya Zambia (Chipolopolo) ambayo ni mabingwa wa Afrika,
Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa
Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ), wachezaji hao ni
Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy
Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis
Kasonde.
Wengine
ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga,
Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses
Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri,
Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
MICHUANO YA KOMBE LA UHAI KUANZA KESHO
Michuano
ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya
miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho
(Desemba 11 mwaka huu) kwenye viwanja viwili tofauti.
Viwanja
vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.
Timu
hizo zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo
itakayomalizika Desemba 23 mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal
Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans.
Kundi
B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba,
wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda
kundi C.
Mechi
za fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2
asubuhi- Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi
B ni African Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam
vs Mgambo Shooting (saa 10 jioni- Chamazi).
Kundi
C litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza
na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting
zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment