Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt,Hussein Mwinyi,akimsalimia Mkurugenzi wa zamani wa TFDA,Margareth Ndomondo (kulia).
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt,Hussein Mwinyi, akipata maelezo alipotembelea Maabara za TFDA.
Wafanyakazi Viongozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA,wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt,Hussein Alli Mwinyi (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo (wa tatu kulia) alipotembelea Maabara wakati wa kutoa Tamko la Wizara hiyo kuhusu Maabara ya Chakula na Mikrobiolojia kupata Ithibati kwa Kiwango cha Kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005.Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TFDA,Balozi Dkt,Ben Moses (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Maabara,Charys Ugullum (wa pili kulia) pamoja na Meneja Uchunguzi wa Chakula,Rajabu salim Mziray. Ghafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt,Hussein Alli Mwinyi (katikati) akionesha Cheti pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Hiiti Sillo (kulia). wakati wa kutoa Tamko la Wizara hiyo kuhusu Maabara ya Chakula na Mikrobiolojia kupata Ithibati kwa Kiwango cha Kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005,Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt,Ayoub Magimba. Ghafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt,Hussein Alli Mwinyi (katikati) akikata Utepe na kufungua Cheti wakati wa kutoa Tamko la Wizara hiyo kuhusu Maabara ya Chakula na Mikrobiolojia kupata Ithibati kwa Kiwango cha Kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005,Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Dkt,Ayoub Magimba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Hiiti Sillo.Ghafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam
Wafanyakazi wa TFDA na Viongozi wao wakiwa na viongozi wa Serikali na Wageni waalikwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya Tamko la Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu Maabara ya Chakula na Mikrobiolojia kupata Ithibati kwa Kiwango cha Kimataifa cha ISO/IEC 17025;2005.
No comments:
Post a Comment