DAR ES SALAAM.
Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inamaliza mwaka 2012 na mafanikio lukuki ikiwa
imeweza kuiletea nchi ya Tanzania mapambano makubwa ya kimataifa zaidi ya
matano.
Haya ni mafanikio ambayo yanapaswa kusifiwa na watanzania wote wapenda
maendeleo kwani kutokana na mapambano hayo nchi imeweza kujulikana kimataifa,
vivutio vyake vya utalii vimeweza kujulikana, nchi imeweza kuwatengenezea
vijana ajira, na kuweza kupunguza uhalifu kwa kuweza kuwapa vijana kazi kwani kukaa
kwao bure ni kishawishi tosha cha kutumia nguvu zao kwa shughuli ambazo sio za maendeleo.
Katika mwaka
unaoishia Desemba 31, 2012, TPBC imeweza pia kuwapeleka nje mabondia zaidi ya
15 wakiiwakilisha nchi ya Tanzania ambako waliweza kuitangaza nchi ya Tanzania vizuri
na kuwavutia wageni wakitalii na kuwekeza katika nchi hii inayojulikana kama
kisiwa cha amani katika bara la Afrika.
Aidha, TPBC
imeweza kuhudhuria mikutano mitatu mikubwa ikiwa ni pamoja na mkutano wa Bodi
ya Wakurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) katika jiji la
London, Uingereza na ule wa mwaka wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola
uliofanyika nchini Bahamas.
Kadhalika TPBC
iliwakilishwa kwenye mkutano wa 30 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chana
cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA)
uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii nchini Marekani
pamoja na ule wa Baraza la Ngumi la Dunia (WBC) uliofanyika pia katika
mjiji la Las Vegas, nchini Marekani.
Hapa nyumbani
, TPBC iliweza kutoa vibali na kusimamia mapambano mengi yaliyofanyika katika
miji ya Tanga, Dar-Es-Salaam, Morogoro, Songea, Mbeya, Morogoro na Arusha na
kuweza kuwapatia mabondia wengi wa
kitanzania mikanda ya Kanda, Taifa na Afrika ya Mashariki, Kati na bara la Afrika.
TPBC inawashukuru
na kuenzi michango ya mapromota wote
waliochangia kuandaa mapambano haya wakiwa ni pamoja na:
Kitwe
General Traders, Kaike Siraju Boxing Promotions, Kyando Boxing Promotions, Mwanzoa Boxing
Promotions, International Boxing Promotions, Selemani Siminyu, Green Hills (T) Limited na wengine wengi.
Aidha TPBC
inapenda kuishukuru TPBO chini ya Abdalla Mwaipaya Ustaadh kwa ushirikiano wake
katika kuendeleza ngumi za kulipwa Tanzania.
Tunapenda
pia kuwashukuru wadau wote waliochangia kwa njia moja au nyingine kama vile
vyombo vya habari, mamlaka za miji na miji na majiji, jeshi la polisi, kumbi zote za
burudani zilizotumika kuandaa mapambano haya na wadau wengine wengi.
Pia tunaishukuru
serikali kupitia Msajili wa Vyama (Mambo ya Ndani), Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Michezo na Katibu Mkuu wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano wao katika kusaidia kuendeleza ngumi za kulipwa nchini.
Imetolewa na:
Onesmo Ngowi
Rais, TPBC
Dar-Es-Salaam,Tanzania
No comments:
Post a Comment