Mkuu Uendeshaji Kampuni ya Maxcom Africa Ltd,Ahmed Lussasi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam kuhusu Kampuni ya Maxcom Africa Ltd, ambapo wateja wa Zuku watalipia ada ya kila mwezi kwa kutumia huduma ya Maxmalipo.Kulia ni Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja Maxcom, Maxmalipo, Mwanahamisi Hamisi.Wengine ni Meneja Mkazi wa Zuku Tanzania Ltd, Fadhili Mwasyeba (wa pili kushoto) na Meneja Masoko Msaidizi Zuku Tanzania,Veneranda Raphael, (PICHA NA TANZANIA LIVE BLOG).
Mkuu wa
Uendeshaji Kampuni ya Maxcom Africa Ltd, Ahmed Lussasi,(kulia) akionesha
mashine ya Maxmalipo ya Kampuni hiyo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana wakati wa kutia saini
makubaliano ya Ushirikiano na Kampuni ya Zuku Pay Tv.Wateja wa Zuku watalipia
ada zao za mwezi kupitia huduma ya MaxMalipo.Kushoto ni Meneja Mkazi
Zuku Tanzania Ltd, Fadhili Mwasyeba.(PICHA NA TANZANIA LIVE BLOG).
Televisheni
ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja
na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Zaidi ya hapo,
wanajumuisha chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports,
MGM movies na zinginezo nyingi. Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za
stesheni kama vile Zuku Afrika ambayo huonesha bara la Afrika, Zuku
Maishaambayo huonesha makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli
lukuki za sinema. Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti
Tanzania nzima.
Dar es Salaam.
Kampuni ya Zuku Pay TV imetia saini makubaliano ya ushirikiano na
Maxcom Africa Ltd ambayo itawezesha wateja wa Zuku kulipia ada zao
wakitumia wakala wa MaxMalipo au mashine za kulipia za Maxcom. Uzinduzi
huu ulifanyika katika mkutano na waandishi hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Fadhili Mwasyeba Meneja Mkuu wa Wananchi
Satellite Tanzania, wamiliki wa vingamuzi ya Zuku Pay TV, alisema
"Wateja wetu sasa wanaweza kulipia ada za Zuku Pay TV wakitumia
technoljia mpya ya MaxMalipo . Zaidi ya hapo wanaweza kupata huduma
kutoka mawakala wote wa MaxMalipo kote nchini. Lengo letu kuu ni
kutumikia wateja wetu na kuboresha huduma zetu. Makubaliano yetu na
MaxMalipo ni ushahidi wa dhamira yetu kuwatumikia wateja wetu.”
Mkuu wa
Uendeshaji Kampuni ya Maxcom Africa Ltd, Ahmed Lussasi, alisema "Tunafurahia
kuingia makubaliano na kampuni ya Wananchi Sattellite, inayotoa huduma
za Zuku Pay TV na kuhudumia wateja wao wote kote nchini. Kampuni yetu
inayo mawakala zaidi ya 3500 nchini na huduma yetu mpya ya malipo kwa
kutumia mashie maalumu za Maxmalipo inatuwezesha tuwafikie hata wateja
katika pembe mbalimbali za nchi. Lengo letu kuu ni kuleta malipo ya
elecktroniki karibu na Watanzania. "
Sasa
kulipia huduma imerahishwa kwa wateja. Wateja wanatakiwa kuwa na Zuku
Subscription ID, kuchagua kati ya huduma ya Zuku Classic, Zuku Premium,
Asia Classic au Asia Premium na huduma ya Zuku inawezeshwa papo hapo.
Zaidi ya hapo, Zuku Pay TV sasa wana promosheni ya "Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure". Programu
hii ya inayowazawadia wateja, itahitaji wateja wa Zuku kuungananisha
wateja kumi (10) wapya au kuunganisha wateja watano (5) wateja wapyana
unashinda televisheni ya inchi 42 na inchi 22. Programu hii hiana draw
na ushindi ni wa uhakika.
No comments:
Post a Comment