Mjumbe wa NEC ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha Mafundi seremala kiitwacho Kazimoto kilichoko kaika mji wa Matai wilayani Kalambo.
Mara baada ya kuzindua matawi hayo mawili ya wakererketwa wa CCM, Mama Salma Kikwete anaonekana akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe hiyo huko Matai katika wilaya Kalambo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Matai waliofurika katika eneo la soko jipya mjini hapo ili kushiriki katika sherehe ya kukabidhi pikipiki kumi kwa ajili ya watendaji wa vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa baadhi ya vikundi vilivyoshiriki katika shughuli ya kukabidhi pikipiki kwenye vituo vya afya vya mikoa ya Rukwa na Katavi zilizofanyika huko Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Matai waliohudhuria sherehe ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Matai waliohudhuria sherehe ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi funguo za pikipiki Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Ndugu Paza Mwamlima kwa ajili ya vituo vya afya vya mkoa huo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Pikipiki hizo zimetolewa na kampuni ya Waterrids.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini ndugu Maria Chambanenji, 38, ambaye ni mlemavu wa ngozi kutoka katika kijiji cha Mkoe, Kata ya Mnyangalua wilayani Sumbawanga ambaye alivamiwa na watu wasiojulikana tarehe 10.2.2013 na kumkata mkono wa kushoto. Maria amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Rukwa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga waliokusanyka katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Theresia.
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Rukwa pamoja na wananchi wakiangalia baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa na Mama Salma. (PICHA NA JOHN LUKUWI)
Na Anna Nkinda –
Sumbawanga
Watoto wa kike nchini wametakiwa kuepukana na vishawishi vya chips Kuku, lifti, simu za mkononi na zawadi za aina mbalimbali wanazorubuniwa nazo kwani vitu hivyo havina nia njema ya kumkomboa msichana kielimu , kijamii na kiuchumi zaidi ya kumuharibia mpango mzima wa maisha yake.
Watoto wa kike nchini wametakiwa kuepukana na vishawishi vya chips Kuku, lifti, simu za mkononi na zawadi za aina mbalimbali wanazorubuniwa nazo kwani vitu hivyo havina nia njema ya kumkomboa msichana kielimu , kijamii na kiuchumi zaidi ya kumuharibia mpango mzima wa maisha yake.
Onyo hilo limetolewa
jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanafunzi wa kike
zaidi ya 1000 kutoka shule mbalimbali za mkoa wa Rukwa katika viwanja vya shule ya Sekondari ya wasichana
ya mtakatifu Theresia iliyopo mjini Sumbawanga.
Mama Kikwete ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kwamba watoto wengi
wa kike wanashindwa kumaliza masomo na kufikia malengo kutokana na
changamoto zinazowakabili ambazo nyingi
siyo za kitaaluma japo zinaathali nyingi kitaaluma , kiafya na kimaendeleo.
“Tunafahamu kuwa
wanafunzi wengi hupata vishawishi ambavyo huwapelekea kupoteza umakini,
muelekeo na kuwa watoro, kupata ujauzito, maambukizi ya Ukimwi na hatimaye
kupoteza fursa hii adimu na adhimu ya elimu ya Sekondari na dira ya maisha yao.
Ni muhimu kujidhatiti na kujiepusha na mitego, vishawishi na matendo yanayoweza
kusababisha matatizo haya.
Msikubali vishawishi kwani
peremende ya dakika si sawa na asali ya maisha.Iweje uridhie kuuharibu mpango
wa maisha yakokwa kitu cha mara moja? Licha tu ya kuwa atakayehusika na kosa la
kukupa mimba anapaswa kushtakiwa kisheria, lakini kwako wewe ni hatari
kiafya kwani kushika mimba ukiwa na umri
mdogo unahatarisha maisha yako wakati wa kujifungua. Asilimia ishirini ya vifo
vya akina mama wajawazito hutokana na uzazi katika umri mdogo”, alisema Mama
Kikwete.
Aidha Mama Kikwepi pia
aliwataka wanafunzi hao kuwatii wazazi wao,kusoma kwa bidii na kujiamini kwamba
wanaweza kwani chochote anachoweza kufanya mtoto wa kiume kitaaluma na
halikadhalika mtoto wa kike anaweza kukifanya hivyo basi wasome zaidi masomo ya sayansi na hisabati kama watoto
wa kiume.
Akisoma taarifa ya
shule ya Sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Theresia Sr. Beatrice Cromweli
ambaye ni mwalimu alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa na shirika la masista wa
Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika Jimbo la Sumbawanga mwaka 2007 ikiwa na
wanafunzi 85 na hadi sasa kuna wanafunzi 489 na walimu 16.
Alisema kuwa lengo kuu
la kuanzishwa kwa shule hiyo ni kuwaendeleza watoto wa kike kielimu na
kimaadili ili kuwakomboa katika unyanyasaji dhidi ya mwanamke na hivyo kuwapa
uwezo wa kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao.
Sr. Cromweli alisema,“Shule
yetu imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi kila mwaka hii hutokana na
ongezeko la vyumba vya madarasa, mabweni ya kulala, vifaa vya kufundishia,
walimu na vitendea kazi mbalimbali na ufaulu mzuri wa wanafunzi katika mitihani
ya kidato cha nne”.
Alizitaja changamoto
zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa vifaa vya maktaba ya kisasa kwani ujenzi wa jengo hilo ambalo halijaanza kutumika kikamilifu
kutokana na ukosefu wa vitabu, meza, viti na kompyuta umeshakamilika, jengo la
bwalo la chakula na ukumbi wa mikutano bado halijakamilika kwani halina meza na
viti na uhaba wa vifaa vya maabara ambavyo vinawafanya wanafunzi kutofanya
majaribio ya kuridhisha.
Mkoa wa Rukwa umekuwa
ukikabiliwa na changamoto ya kushuka kwa
kiwango cha elimu hasa kwa mtoto wa kike , karibu asilimia 39 ya watoto hao
huacha shule kabla ya kumaliza elimu ya Sekondari kutokana na tatizo la utoro,
ujauzito na wazazi kutotilia maanani suala la elimu.
No comments:
Post a Comment