Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Dk,Anacleti Kashuliza (kushoto)akizungumza,Mwengine ni Mkurugenzi Mwendeshaaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),Gidion Nasari.
Wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini.
NEEC
na NDC wasaini makubaliano ya ushirikiano wa
kuwawezesha wananchi kiuchumi
Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) wameanzisha ushirikiano utakaowawezesha wananchi kiuchumi
katika maeneo ambayo NDC imeanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo. Manufaa
haya kwa wananchi yanatokana na kusainiwa kwa Makubaliano ya ushirikiano kati
ya mashirika haya ambao unalenga kutoa fursa kubwa za ushiriki wa kiuchumi kwa
wananchi wa maeneo husika.
Hadi
sasa, miradi inayolengwa ambayo inasimamiwa na NDC ni uchimbaji wa Makaa ya
Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga Wilayani Ludewa unaotekelezwa chini ya
Kampuni ya ubia ya Tanzania China International Minerals Resources Limited
ambao unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 5000 kwa watanzania ambazo ni fursa kubwa ya kukuza mapato ya
wananchi wa Ludewa.
Matarajio
ya NEEC na NDC ni kuwaendeleza na kuwawezesha kiuchumi wananchi walioko katika
maeneo ambayo miradi imeanza
kutekelezwa ili waweze kujipanga na kujiandaa vema kufaidika na fursa hizo kwa
kufanya yafuatayo:-
- Kutoa mafunzo ya ujengaji uwezo na ujuzi katika kutambua fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia,
- Kuhamasisha fursa na miundo mbinu ya kiuchumi,
- Kuhamasisha kujiunga katika Mitandao ya Vikundi na Masoko,
- Uwezeshwaji wa Upatikanaji wa Mitaji na kuunganishwa na Taasisi za Fedha,
- Kuainisha na Kuendeleza maeneo huru ya Kufanyia Biashara na
- Kuhamasisha Umuhimu wa Ushirika
Lengo
la makubaliano ya ushirikiano huu ni kuweka mifumo ya utekelezaji na usimamizi
wa kuwaendeleza na kawawezesha wananchi katika maeneo ya miradi mbali mbali
inayosimamiwa na Shirika la Taifa la
Maendeleo ili waweze kunufaika vema na rasimali asilia zinazowazunguka.
Taasisi
hizi mbili zinatarajia kushirikiana vema katika
kuwaunganisha wadau mbali mbali wa maendeleo katika maeneo husika
hususani wawekezaji wa sekta binafsi,mashirika yasiyo ya kiserikali,wadau wa
maendeleo na serikali za mikoa na wilaya katika kuwaendeleza na kuwawezesha
wananchi katika maeneo husika.
Ni
matarajio ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Shirika
la Taifa la Maendeleo (NDC) kuona rasilimali asilia zikiwanufaisha wananchi
katika maeneo yao kwa kuwawezesha kushiriki kwa kiasi kikubwa katika shughuli
za kiuchumi na kubadili hali zao za maisha kupitia ongezeko la kipato na
kuboreka kwa miundombinu.
Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilianzishwa chini ya kifungu
cha nne (4) cha Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi . Baraza
lilianza kazi rasmi mwaka 2005 likiwa ni chombo cha juu cha kusimamia
utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ni chombo cha umma
kinachomilikiwa asilimia 100 na Serikali, Shirika hilo lililoanzishwa mwaka
1965 kuchochea maendeleo ya nchi kupitia viwanda katika sekta zote za uchumi.
Imetolewa na:-
Dk Anacleti Kashuliza
Gideon Nasari
Katibu Mtendaji
Mkurugenzi Mwendeshaji
Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Shirika La Maendeleo La Taifa
Dar es Salaam
Tarehe: 15 Februari, 2013
No comments:
Post a Comment