Afisa
Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi
karibuni katika ukumbi wa Karimjee zawadi ya redio (music sytem)
Winfrida Leonard kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya
WAMA – Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya
tatu katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake
kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa
wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo
jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
Faiza Ussi kutoka
shule ya Sekondari ya Sunni Madressa ya mjini Zanzibar alifurahia
zawadi ya laptop aliyopewa hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee mara
baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuandika insha
kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo
yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa
ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
Washindi kumi walioshiriki shindano
la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania
lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa
ufadhili wa Japan (JATA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki
katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo
mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za
kimarekani.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika
picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya
Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki shindano
la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania
lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa
ufadhili wa Japan (JATA) nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki
katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo
shule ya WAMA-Nakayama aliibuka mshindi wa jumla.
Meneja wa shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama Ali
Mindria (kulia) akipokea kombe la ushindi hivi karibuni katika ukumbi
wa Karimjee kutoka kwa Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda
(kushoto) baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika shindano
la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania
lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa
ufadhili wa Japan (JATA). Wanafunzi wane kutoka shule hiyo waliingia
kumi bora kwa kushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa kati ya
wanafunzi 32 walioshiriki shindano hilo. (Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
No comments:
Post a Comment