MAREHEMU MWL.ADELINA AMBROSE NKWITA.
SHUKRANI.
Familia ya Mzee Issa Nakaunda Mangosongo
inapenda kutoa shukrani kubwa kwa wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine
katika msiba wa mama yetu mpendwa Mwl. Adelina Ambrose Nkwita, pichani hapo juu.
Shukrani hizo
ziwaendee madaktari wa Hospitali za
Mikocheni, Muhimbili na Regency kwa
juhudi za kuokoa maisha ya marehemu mama yetu
aliyefariki dunia tarehe 10/05/2013 na kuzikwa tarehe 13/05/2013 katika makaburi ya Tabata Segerea.
Si rahisi
kumtaja kila mtu, shukrani zingine ziende kwa Manispaa ya Ilala, Shule ya
Msingi Olympio, Chama Cha Walimu Tanzania, Tawi la Manispaa ya Ilala,Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Parokia ya Kristu Mfalme, Kwaya ya Parokia
ya Kristu Mfalme, Jumuiya ya Mt.Don
Bosco ,ndugu, jamaa na marafiki.
Misa ya shukrani
kwa ajili ya kumwombea marehemu itakuwa
Jumamosi tarehe 22/06/2013 saa 12.15 asubuhi katika Kanisa la Kristu
Mfalme, Tabata.
Lakini
katika mambo hayo yote tunayoshinda na zaidi ya kushinda, kwa yeye
aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika kwamba wala mauti, wala uzima,
wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala
wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala chini, wala kiumbe kingine chochote
hakitaweza kututenganisha na upendo wa MUNGU ulio katika Kristo Yesu
Bwana wetu, WARUMI 8:37-39.
Amina.
No comments:
Post a Comment