Na Anna Nkinda - Yokohama
Watumiaji wa lugha ya
Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia hatua ya kuwa na
mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka kilichopo nchini humo.
Hayo
yamesemwa leo na Prof. wa chuo hicho Midori Uno wakati akiongea na Mke wa
Rais mama Salma Kikwete alipokutana naye katika hoteli ya Intercontinental mjini
Yokohama.
Prof. Uno ambaye ni Mwalimu wa kiswahili katika chuo hicho alisema kuwa hivi Sasa wananchi wengi wa
Japani wanakiu ya kujifunza na kuzungumza lugha ya Kiswahili kwani ni rahisi kueleweka.
“Katika jitihada zangu za kuwafanya
wajapani wengi wajue lugha ya Kiswahili nimetengeneza kamusi ya maneno ya kijapani kuwa ya Kiswahili ambayo watu wengi wanaitumia kwa
sasa kwani wengi wajapani wengi wanapenda kujifunza lugha hii”, alisema Prof. Uno.
Mashindano hayo ya lugha ya Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila
mwaka huwa ni ya kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa
cheti, tuzo ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake Mke wa Rais mama Kikwete alimpongeza profesa huyo kwa jitihada
zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini
humo na kumuomba aendelee zaidi kufanya hivyo.
Alisema kuwa watanzania wanavitu vyao vya kujivunia
kama Taifa, moja ya vitu hivyo ni lugha
ya Kiswahili ambayo imewaunganisha
watanzania wote na kuwa kitu kimoja ndani na n je ya nchi.
Mama Kikwete alisema, “Ili kumfikia mtu mmoja au watu
wengi zaidi ni lazima kuwe na lugha ya mawasiliano hivyo basi nasi
tunatumia lugha hii ambayo iliwaunganisha watanzania wote wakaweza kupigania
uhuru wa n chi yao kipindi cha mkoloni”.
Alisema kuwa lugha ya Kiswahili inaongelewa maeneo
mengi ya Afrika ya mashariki na ndani ya bara la Afrika na hivi sasa viongozi
wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) waliikubali lugha hiyo kuwa lugha ya
mawasiliano .
Profesa Uno alikuja nchini kabla ya kupata uhuru kwa ajili ya kufanya kazi za
kujitolea na aliporudi nchini kwake aliamua kuwafundisha wajapani lugha ya
Kiswahili pia nchini humo redio Japani (NHK)
inatangaza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilianzishwa
mwaka 1964.
No comments:
Post a Comment