Hiki
ndicho kikosi kamili cha timu ya benki ya NMB kilichong’ara siku hiyo katika
kutimua kivumbi kwenye uwanja wa jamhuri.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mhe. George
Mkuchika ambae alikua ndiye mgeni rasmi akikagua kikosi cha timu ya NMB kabla ya mpambano huo.
Kikosi cha timu ya waheshimia wabunge iliyowatikisa wachezaji wa timu ya NMB.
Hawa ni sehemu ya mashabiki wa timu hizi mbili wakifuatilia na wakifurahia
mtanange huo.
Naibu waziri wa habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Amos Makalla (katikati) akipigwa chenga na Afisa mkuu wa fedha NMB, Waziri Waziri, katika mtanange huo uliokuwa wa kukata na shoka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma mwishoni mwa wiki.Wabunge waliibuka washindi kwa bao 1-0.
Katika kuendeleza na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya
Benki ya NMB na waheshimiwa wabunge, Benki ya NMB iliandaa mtanange wa kukata
na shoka ambao ulihudhuriwa na washabiki wa timu hizo mbili ambao ni wakazi wa manispaa ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment