Na Anna Nkinda –
Maelezo
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete amewataka wanawake wa dini zote nchini kutokubaguana
kutokana na itikadi zao za vyama vya siasa bali wawe mstari wa mbele
kuhubiri amani na upendo.
Mama Kikwete aliyasema hayo
jana wakati akiwafutarisha wanawake wa
dini mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete alisema
kuwa ukosefu wa amani ukitokea katika nchi wanawake na watoto ndiyo wahanga
wakubwa hivyo basi wasikubali watu kuwadanganya bali wawe na msimamo na
umoja ili waweze kuilinda amani ambayo ndiyo silaha pekee ya kuwaletea
ukombozi iliyoasisiwa na wazee wa nchi
yao.
“Ninawashukuru kwa
kuacha shughuli zenu na kuitikia wito wangu wa kuja na kufuturu pamoja nami,
nawatakia mfungo mwema nini nyote mnaofunga ili Mwenyezi Mungu awakubalie heri
zenu nanyi msiofunga Mwenyezi Munguawabariki katika maisha yenu ya kila siku”,
alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa
Kiislamu Tanzania Taifa (BAKWATA) Shamim
Khan alimshukuru Mama Kikwete kwa upendo wake wa kuwaalika wanawake hao kupata
futari ya pamoja.
Mama Khan alisema kuwa
kukutana kwao kumewafanya wajifunze kuwa wakitaka amani ni lazima washirikiane
bila ya kujali rangi, dini na kabila kwani wanawake wote wanamatatizo yanayofanana
ambayo wanaweza kuyatatua kwa pamoja bila ya kuangalia kuwa huyu ni mkristo au muislamu na wakikaa pamoja amani inapatikana.
Naye Olive Lwema ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya
Wanawake wakristo Tanzania alisema kuwa aliposikia wamepata mwaliko huo
alifurahi sana kwasababu wanapokutana wanawake ambao ni wazazi wa watoto wa
taifa, wake wa waume wanaoongoza nchi hakuna jambo litakaloharibika na
ameshuhudia kwa kuona nyuso za ushirikiano na upendo baina yao.
Mama Lwema aliwaomba
wanawake wanaofunga kipindi hiki cha
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wajitoe kufunga kwao kwa ajili ya maombi maalum ya
kuombea amani na watoto kwani hivi sasa vijana wengi wanaomaliza vyuo hawana ajira, shule haziendi sawa na
wanaopata machungu ya haya yote ni wanawake.
No comments:
Post a Comment