Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa VETA
Idrisa Mshoro (katikati)akipewa maelezo na Alfan Ngowo juu ya Teknolojia
za ukusanyaji wa taarifa za ardhi na mazingira wakati alipotembelea
katika banda la VETA lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam.kulia niMkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi na Makamu
Mwenyekiti wa Maonesho wa VETA Abduri Mollel.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi wakati alipotembelea
katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho
katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliofika katika banda la
VETA wakipata maelezo kutoka kwa Theopista Michael ambaye ni mwanafunzi wa chuo
VETA cha Njiro Arusha kinachotoa mafunzo ya Diploma ya mambo ya hoteli na
utalii.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue akipewa maelezo na Mwalimu wa VETA Tabora Diana Mlengeki juu ya
mashine ya useketaji wa nguo aina mbalimbali zitokanazo na nyunzi wakati
alipofika katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali zinazotplewa na
Chuo hicho katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
VETA Idrisa Mshoro (katikati)akimsikiliza Mkufunzi wa madereva Anthony
Gaspar wakati alipokuwa akimuelezea njinsi ya madereva wanavyoweza kuzuia ajari
baada ya kupewa mafunzo wakati alipotembelea katika banda la VETA
lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.kulia
niMkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi na Makamu Mwenyekiti wa
Maonesho wa VETA Abduri Mollel
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi
na Ajira Eric Shitindi akimsikiliza Linda Njenje ambaye ni mwanafunzi
mwenye mahitaji maalumu anayesoma katika chuo cha VETA kwa walemavu kirichopo
Usariva Arusha,akitoa maelezo juu ya mafunzo wanaoyoyapata katika chuo hicho
wakati alipotembelea katika banda lao lililopo kwenye maonesho ya 37 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya
Tanzania Mh.Fakih Jundu (katikati) akizungumza.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya
Tanzania Mh.Fakih Jundu (kushoto) akimsikiliza mwalimu wa VETA Morogoro
Sophia Tuka wakati alipokuwa akimuelezea juu yautengenezaji wa alama za
barabarani ,zilizotengenezwa na wanafunzi wa VETA,Kulia niniMkurugenzi Mkuu wa
VETA mhandisi Zebadiah Mosh na Kushoto niMsajili wa Mahaka Kuu Benedict
Mwingwa.
No comments:
Post a Comment