NSSF YATOA SOMO KWA WAJASIRIAMALI ILI WAISHI MAISHA BORA.
Ofisa
Uendeshaji Mwandamizi wa Sekta Isiyo Rasmi wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Khalfan akifafanua jambo kuhusu huduma
wanazotoa wakati wa uzinduzi wa Ushirikiano wa Kikazi kati ya Umoja wa
Wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi, NSSF, Equity Bank na Sanitas Hospital
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mlezi wa umoja huo,
Ramadhani Madabida na Meneja wa Huduma za Wateja wadogo wa benki ya
Equity, Janeth Zoya. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakiwa katika uzinduzi huo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKA
La Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeupongeza Umoja wa Wafanyakazi
wa Sekta Zisizo Rasmi (Informo Sector Workers Union -ISWU), huku
likiwataka kutumia vema fursa itokanayo na unganiko la kikazi baina ya
umoja huo, NSSF, Equity Bank na Sanitas Hospital.
Wito
huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Sekta
Zisizo Rasmi wa NSSF, Salim Khalfan, alipokuwa akizungumza na wanachama
wa ISWU walioshiriki semina na uzinduzi wa ushirikiano huo chini ya programu ya ‘Community Cooparetive Micro Insuarance (CCMI).’
Khalfani
aliuambia umoja huo kuwa, NSSF inampongeza Mkurugenzi wa Umoja wa
Wafanyakazi wa Sekta Zisizo Rasmi, Dauda Wadauda kwa kuratibu umoja huo
na kwamba shirika lake liko tayari kusaidiana katika kuwawezesha kufikia
malengo yao kibiashara.
Aliongeza
kuwa, uwezo mkubwa wa kusaidia harakati za afya na matibabu kwa
wajasiriamali iliyonao shirika lake ulikuwa unakosa nguvu ya kuwafikia
mmoja mmoja miongoni mwa wajasiriamali na kwamba kuungana kwao
kunarahisisha NSSF kuwafikia na kuwawezesha.
“Wanachama,
mnapaswa kutumia fursa hii kwa kuwekeza kadri muwezavyo pesa zenu
katika shirika letu, ili kunufaika na huduma za NSSF, ambayo kwa
kushirikiana na Equity Bank na Sanitas Hospital, iko tayari kukabili
changamoto zenu za ndani na nje ya ujasiriamali.
Kwa
upande wake, Mlezi wa ISWU, Ramadhani Madabida, aliishukuru NSSF kwa
kukubali kuungana katika vita dhidi ya umaskini ambao aliutaja kama moja
ya vyanzo vinavyochangia ukosefu wa amani katika nchi yoyote duniani na
kwamba amani ni uwezo wa kukabiliana na changamoto.
Mkurugenzi
wa ISWU, Dauda Wadauda, aliwataka wajasiriamali hao kutumia vema elimu
waliyopata katika semina hiyo na kuwataka wawe mabalozi wazuri kwa
wajasiriamali walio nje ya umoja huo ili kuongeza idadi yao na kuwa na
nguvu ya pamoja.
No comments:
Post a Comment