Na Frank Geofray-Jeshi
la Polisi, Windhoek Namibia.
Timu ya mpira wa miguu
ya Polisi Tanzania inayoshiriki michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa nchi za
kusini mwa Afrika (SARPCCO) imeanza vibaya baada ya kupoteza mchezo wake wa
kwanza dhidi ya timu ngumu na bingwa mtetezi Polisi Zambia baada ya kukubali
kichapo cha mabao 2 -1 katika mchezo
uliochezwa jana usiku katika uwanja wa taifa wa Namibia.
Mabao ya Zambia
yalifungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Musukuma Chipunga katika dakika
ya 15 na 20 baada ya uzembe uliofanywa
na safu ya ulinzi wa timu ya Polisi Tanzania.
Bao la Tanzania
lilipatikana kipindi cha pili kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya kuangushwa
kwa John Kanakamfumu katika eneo la hatari wakati akipokea pasi iliyopigwa na
Saimon Lezire.
Penati hiyo iliwekwa
kimiani na John Kanakamfumu baada ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa
Zambia ambaye jana alikuwa mwiba kwa Polisi Tanzania baada ya kuokoa mashuti
yaliyokuwa yakipigwa na wachezaji wa Tanzania.
Hata hivyo kipindi cha
kwanza Polisi Tanzania haikucheza vizuri hadi kipindi cha pili baada ya kuingia
kwa Delta Thomas, Madope Mwingira na
John Kanakamfumu ambao walionyesha uhai kwa timu ya Tanzania.
Katika Mechi nyingine
ya kundi A, Polisi Zimbabwe ilishinda 2-1 dhidi ya Afrika kusini.
Wakati huohuo
Wanariadha wameendelea kuipatia Tanzania Medali baada ya kuibuka mabingwa
katika mbio za mita 5000, 1500 na washindi wa pili katika 5000 na kurusha tufe.
Waliopata medali jana
ni pamoja na Fabian Nelson 5000 (Dhahabu), Basil John 1500 (Dhahabu), Wilbardo
Peter 5000 (Fedha),Mohamed Ibrahimu
katika kurusha tufe (Fedha) na Basil John tena (Shaba) katika mbio za
vijiti.
No comments:
Post a Comment