Wanawake mkoani Iringa wametakiwa kuitumia Hospitali ya rufaa ya mkoa huo kupata huduma ya uzazi pamoja na watoto wao na kuachana na tabia ya kujifungulia majumbani, kupeleka watoto kwa waganga wa jadi kwa kudhani kuwa magonjwa wanayoumwa hayawezi kutibika Hospitalini.
Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua jengo la huduma za watoto katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambayo imejengwa kwa msaada wa Hospitali rafiki ya Vicenza iliyopo katika mkoa wa Veneto nchini Italia.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuna baadhi ya wazazi wakiona watoto afya za watoto wao zinadhoofika ikiwa ni pamoja na kuumwa ugonjwa wa utapiamlo wanadhani kuwa jirani zao wanawaonea wivu na kuwaroga na wanaona njia sahihi ni kwenda kwa waganga wa jadi badala ya kuwapeleka Hospitali ili wakaonane na wataalamu wa afya.
Alisema vifo vya watoto
wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa sasa ni 54 katika kila watoto
wanaozaliwa wakiwa hai 1000 na katika mkoa huo idadi ya vifo hivyo ni watoto 20
kwa kila vizazi hai 1000 nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vifo hivyo vinapungua
ili kuweza kufikia malengo ya Maendeleo ya Milinia ifikapo mwaka 2015.
Aidha Mama Kikwete pia
aliwataka wakazi wa mkoa huo kujiepusha na mazingira yawatayowapeleka kupata
maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kuwa waaminifu katika ndoa zao na kwa wale
ambao hawana ndoa watulie na kujitunza huku wasubiri muda wao wa kuoa au
kuolewa ukifika.
“Mkoa huu maambukizi ya
Virusi Vya Ukimwi (VVU) yako juu takwimu zinaonyesha kuwa watu tisa kati ya 100
wanamaambukizi , hivyo basi nawasihi mjitunze na kuheshimu ndoa zenu kwa
kufanya hivyo hamtaweza kupata maambukizi ya ugonjwa huu kirahisi ingawa
unaweza ukapata kwa njia nyingi lakini maambukizi mengi yanapatikana kwa njia
ya kufanya mapenzi yasiyo salama”, alisema Mama Kikwete.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma aliushukuru uongozi
wa mkoa wa Veneto na Hospitali ya Vicenza kwa msaada wa ujenzi wa wodi ya
watoto na ujenzi wa jengo la kujifungulia kina mama wajawazito.
Dkt. Ishengoma aliahidi
atahakikisha na kusimamia ili jengo hilo
liweze kutumika kama lilivyokusudiwa na
wahudumu wa Hospitali hiyo waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.
Akisoma taarifa ya
ujenzi wa jengo hilo mganga mkuu wa mkoa Dkt. Robert Salim alisema jengo hilo
ni awamu ya pili ya ujenzi kwani awamu ya kwanza ilikuwa ni ujenzi wa jengo la
kujifungulia wajawazito ambalo kwa kiasi kikubwa limeboresha huduma na kupuza
vifo vya wazazi na watoto wachanga.
Dkt. Salim alisema lengo la kujengwa kwa wodi ya watoto ni kuboresha huduma ya afya, kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vinavyotokana na magonjwa ya kuambukiza na kupunguza msongamano katika wodi ya watoto.
"Faida za mradi huu ni kuboresha utoaji wa huduma kwa urahisi kwa watoto wagonjwa kwa kuwa na eneo kubwa la kufanyia kazi, kupunguza msongamano na kutatua tatizo la wagonjwa kulala wawili wawili au zaidi katika kitanda kimoja.

Pia ni kupunguza
maambukizi ya magonjwa kwa watoto waliolazwa , kuwa na eneo la kutolea elimu ya
lishe kwa watoto na kuwapatia watoto eneo la michezo na kupenda kusoma",
alisema Dkt. Salim.
Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini Luigi Scotto aliwashukuru watu wote waliohusika hadi kukamilika kwa mradi huo na kusema anajivunia kuwa balozi katika nchi ya Tanzania yenye ambayo watu wake ni wakarimu na wenye ushirikiano wa hali ya juu.
Kukamilika kwa mradi huu ambao ni moja ya kazi zinazofanywa na n chi ya Itali hapa Tanzania inaonyesha mahusiano mazuri ya kirafiki ambayo yalikuwepo kwa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili nitaendelea kuhakikisha kuwa tunaimarisha sekta ya afya hapa nchini ili watanzania wapate huduma bora”, alisema Balozi Scotto.
Naye Katibu Tawala (RAS) wa mkoa wa Veneto nchini Italia Roberto Ciambetti alisema uhusiano kati ya hospitali ya Vicenta ya nchini humo na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa mwaka 2003 ukiwa ni muendelezo wa miradi iliyoanzishwa na shirika lisilo la kiserikali la “Doctor with Africa CUAMM” la nchini humo.

Alisema shirika la
Doctor with Africa CUAMM linafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa
na kutengeneza miradi ya afya ya ushirikiano, kuwaleta madaktari bingwa na
wataalamu wengine wa afya katika nchi za Afrika, kuwasomesha madaktari katika
fani za afya, kufanya tafiti za afya na kutekeleza program za uelimishaji
jamii.
Alisema Hospitali ya
Vicenza imekamilisa miradi miwili na a Hospitali ya rufaa ya Iringa ambayo
malengo yake ni kutoa msaada wa kitaaluma
ili kuboresha ubora wa huduma, kuanzisha progeamu ya kubadilishana
wataalamu kati ya pande mbili ili kuboresha zinazotolewa.
Kuisaidia Hospitali ya
Rufaa ya mkoa kupata vifaa vya kisasa na vifaa tiba, kuwasomesha watumishi wa
hospitalikwenye fani mbalimbali ndani nan je ya nchi na kuboresha miundombinu.
Hospitali ya Rufaa ya
Iringa inahudumia wakazi zaidi ya
milioni moja na nusu wa mkoa huo na Njombe pia ina uwezo wa kubeba vitanda 500 lakini
vilivyopo ni 455. Kwa sasa inatoa huduma za kawaida na huduma zinazohitajika
utaalamu zaidi kwa wagonjwa wanaopata rufaa kutoka hospitali za wilaya. Wastani
wa wagonjwa wanaotibiwa kwa mwezi ni 4310 na wanaolazwa kwa siku ni 59.
Kukamilika kwa mradi
huo ni jitihada kubwa iliyofanywa na Baba Askofu wa jimbo katoliki la Iringa Mhashamu Tarciusius
Ngalalekumtwa pamoja na baraza la maaskofu Tanzania (TEC) katika kuanzishwa kwa
uhusiano wa Hospitali hizo mbili na kupendekeza kwa wafadhili kuwepo kwa mradi
wa kuboresha huduma za Mama na mtoto ambao
ulipata fedha za utekelezaji.
Mradi wa ujenzi wa wodi hiyo ya ghorofa moja lenye sehemu mbili za kulaza wagonjwa ulianza mwaka 2010 na kukamilika 2012 umegharimu shilingi bilioni moja milioni mia nane na arobaini na mbili ambazo zimetolewa na Hospitali ya a Vicenza kwa upande wa ofisi ya Mkuu wa mkoa imechangia shilingi milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa mfumo wa maji taka na kujenga mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia maji ya kisima.

No comments:
Post a Comment