TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO
Utangulizi
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma juu ya kuwepo kwa Ugonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo mkoani
Rukwa. Ugonjwa umedhibitika kuwepo
baada ya Vipimo vya Maabara kuonyesha uwepo wa vijidudu vya homa ya uti wa mgongo kwenye sampuli za wagonjwa waliolazwa
kwenye Hospitali ya Mkoa Sumbawanga. Hadi kufikia tarehe 08/10/2013 jumla ya wagonjwa 21 wameripotiwa katika hospitali ya Mkoa
na kati yao wanne ( 4) wamefariki dunia
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu
kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania hususani mikoa iliyo mpakani
na mkoa wa Rukwa na vile vile wasafiri wanaotarajiwa kwenda mkoani Rukwa.
Homa ya Uti wa Mgongo
Homa ya Uti wa Mgongo inasababishwa
na bakteria aitwaye Neisseria
meningitidis. Bakteria huyu
ndiye anayeleta milipuko mikubwa ya Homa ya Uti wa mgongo. Ugonjwa huu hatari
unaathiri zaidi meninji na husababisha athari kubwa kwa ubongo. Ugonjwa huu
unapatikana kwa binadamu tu. Asilimia 50 za wagonjwa hupoteza maisha iwapo
matibabu hayataanzishwa mapema.
Dalili kuu ni Kukakamaa
kwa shingo, Homa kali, Kutokupenda mwanga mkali, Kuchanganyikiwa, Kichwa kuuma
pamoja na Kutapika. Ugonjwa huu unaweza kuathiri ubongo na kupelekea kupoteza
uwezo wa kusikia au kupoteza kabisa uwezo wa kuelewa na kunyambulisha vitu
mbalimbali. Iwapo ugonjwa huu utaathiri ubongo na meninje kwa kiasi kikubwa,
umauti hutokea. Dalili za ugonjwa
ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukizi.
Ugonjwa huu unaenezwa kutoka kwa
binadamu kwenda kwa binadamu kwa njia ya hewa au kwa kugusa majimaji/mate
kutoka kwa mtu ambaye tayari ni mgonjwa. Ugonjwa huu unaenea kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kwa urahisi na kwa
kasi sana iwapo mtu atakuwa karibu na mgonjwa mwenye maambukizi kwa muda mrefu.
Uambukizo unaweza kutokana iwapo mgonjwa atapiga chafya au mate ya mgonjwa huyu
kuguswa. Aidha kasi ya maambukizi pia inatokea iwapo mtu ataishi kwa karibu ndani
ya nyumba moja na mgonjwa na kushirikiana naye kwa kula chakula kwenye chombo
kimoja.
Ugonjwa
huu unatibika iwapo mgonjwa atawahi hospitalini na kupewa dawa.
Hatua zinazochukuliwa na Wizara
·
Kutoa taarifa ya
tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa
Tanzania Bara hususan mikoa inayopakana na Rukwa. Aidha taarifa hii pia imewakumbusha
waganga wakuu warejee miongozo yao ya kudhibiti Ugonjwa wa Homa ya Uti wa
Mgongo yaani namna ya utambuzi wa mgongwa na, uchukuaji wa sampuli
·
Kuimarisha ufuatiliaji
wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya
mipakani.
·
Kutuma Timu ya Taifa ya
Maafa ambayo imeenda kuungana na timu za Mkoa na Wilaya za Rukwa katika
kukabilana na ugonjwa huu. Aidha timu hiyo imeondoka tarehe 10.10.2013
·
Kutuma chanjo pamoja na
dawa na vifaa Kinga kwa mkoa wa Rukwa ili kuweza kukabilana na ugonjwa huu
·
Elimu ya Afya inaendelea kutolewa katika maeneo ambayo yamekumbwa na mlipuko na pia
mashuleni, vyuoni, magerezani, nakwenye mikusanyiko na msongamano wa watu.
Aidha wananchi wanashauriwa kujenga nyumba bora zenye madirisha yanayoingiza hewa
na mwanga wa kutosha
·
Kufungua kambi maalamu
mkoani Rukwa kwa ajili ya wagonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo
Wananchi wanashauriwa kutoa
taarifa pindi kutoa taarifa kwenye kituo cha huduma za
afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na
dalili za ugonjwa huu.
Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii na Wadau wengine wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha ugonjwa huu
unathibiwa mkoani Rukwa na kwa mikoa mengine.
Nsachris Mwamwaja
Msemaji
12 Oktoba 2013
No comments:
Post a Comment