Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akibeba tofali kushiriki ujenzi wa chumba cha, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipewa zawa Salome Mwakalinga kwa niaba ya Kinana mama wa Kata ya Katende, Wilayani Rungwe mkoani Mbeya. |
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipasua ubao, wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) aliposhiriki ujenzi wa vyumba vya maabara, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alishiriki kupasua mbao kwa ajili ya ujenzi huo.
Mzee Issa Simon wa Kata ya Kandete, wilayani Tukuyu mkoani Mbeya, akimsimika Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwa Mzee wa Kinyakyusa, kabla ya mkutano wa hadhara uliofanywa na Kinana katika kata hiyo, katika shule ya sekondari Mwakaleli, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 25, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe. Baada ya kutawazwa alipewa jina la Mwakinana.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akihutubia mamia ya wananchi katika Kijiji cha Kandete, wilayani, Rungwe,akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani humo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipewa zwadi ya kitenge kwa ajili ya mkewe, na kiongozi wa Kinana mama wa Kata ya Kindete,wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Salaome Mwakalinga.
Mamia ya wananchi wa Kata ya Kandete, wilayani Rungwe mkoani Mbeya wakimsikiliza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipohutubia mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata hiyo,
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akisalimia wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kandete, wilayani Rungwe mkoani Mbeya,
Mkazi wa Kijiji cha Kipapa, Kata ya Busokelo, wilyani Rungwe mkoani Mbeya, akishangilia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliposimama kwa muda katika kijiji hicho, Nov 25,2013, Katibu Mkuu akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani humo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kipapa, Kata ya Busokelo, msafara wake ulispomamishwa na wananchi wa Kijiji hicho, Nov 25. 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia za kuzitatua, wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.(Picha na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment