Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete, akivishwa skafu mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Lindi.
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la Jangwani lililoko katika Kata ya Chikonji huko Lindi.
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la Jangwani lililoko katika Kata ya Chikonji huko Lindi.
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kutoka Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akisononeka baada ya kubaini kuwa watoto wengi wanaoonekana katika picha kutoka Kijiji cha Jangwani wamekatisha masomo yao. Mama Salma alikwenda kijijini hapo kuongea na wajumbe wa Halmashauri ya Tawi hilo.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
Na Anna Nkinda –
Maelezo, Lindi
Wazazi mkoani
Lindi wametakiwa kusimamia elimu ya watoto wao kwa kufuatilia mahudhuria yao shuleni jambo
ambalo litawasaidia katika maisha yao ya
baadaye kwa kuweza kujiajiri au kuajiriwa pindi watakapomaliza masomo na hivyo
kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Wito huo umetolewa jana
na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) wakati
akiongea kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya
Chama hicho katika matawi ya Jangwani, Tandangongoro na Mkupama yaliyopo
katika wilaya ya Lindi mjini.
Akiwa katika tawi la
Jangwani lililopo katika kata ya Chikonji Mama Kikwete aliongea na watoto ambao aliwaita ili awasalimie na baada
ya kuwauliza maswali kuhusu elimu walisema baadhi yao waliacha shule kwa ajili ya utoro. Jambo
alilolifanya ni kuwasisitiza watoto hao kusoma kwa bidii na
kuepukana na tabia ya utoro kwani elimu ni ukombozi wa maisha yao.
Baada ya kuongea na
watoto hao ambao wengi wao walikuwa ni wanafunzi wa shule ya Msingi Mjumbe huyo
wa NEC taifa aliongea na viongozi wa CCM na kuwataka wao kama wazazi kutatua tatizo la utoro kwa watoto wa kijiji hicho kwa kusimamia na kuhakikisha wanakwenda shule
kwa wakati.
“Hali ya elimu katika
mkoa wa Lindi ni ngumu vijana hawasomi wengi wao wanakatiza masomo kwa ajili ya
utoro na kuolewa sisi kama viongozi ni
lazima tupige kelele ili kuhakikisha watoto wanakwenda shule na
kuhudhuria masomo darasani”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete pia
aliwaasa viongozi hao wa Halmashauri kuu
ya tawi kutunza amani iliyopo na kuitumia katika shughuli mbalimbali za
maendeleo ikiwa ni pamoja na kulima mazao hasa yanayohimili ukame ikiwa ni
pamoja na mtama ili kuepukana na tatizo
la njaa linaloikabii wilaya hiyo mara kwa mara.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa alisema katika mikoa ya Kusini ambayo ni
Lindi na Mtwara hivi sasa kuna maeneo matatu yanayotoa gesi ambayo inaleta utajiri lakini uchimbaji wake unahitaji vijana waliosoma.
“Uchimbaji wa gesi
unahitaji kupata wataalam ambao wamesoma kama watoto wetu hawatakuwa na elimu
watakuja watu kutoka mbali na kufanya kazi ya uchimbaji wakwetu wataishia
kufanya kazi ya vibarua tu. Nawaomba muwaache watoto wasome msiwaoze au kuwaacha
wanakatiza masomo kwa ajili ya utoro”, alisema Mzee Mtope.
Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC Taifa kupitia
wilaya ya Lindi mjini alikutana na viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya
CCM kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya
vikao na viongozi.
No comments:
Post a Comment