Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja ya wake wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola wanaokutana Colombo nchini Sri lanka mara baada ya ufunguzi rasmi uliofanywa na Prince Charles kwa niaba ya Malkia Elizabeth II kwenye ukumbi wa Nelum Pokuna Mahinda Rajapaksa, ulioko mjini Colombo, nchini Sri lank.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na wake wengine wa wakuu wa nchi za Madola wanaokutana nchini Sri lanka wakitembelea maonesho ya vito yaliyoandaliwa na National Gem and Jewery Authority ya nchini Sri lanka. Katika picha anaonekana Meneja wa City of Gem Museum, Bwana Thushara Ekanayaka akimwonyesha Tanzanite.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mke wa Waziri wa Mambo ya nje wa Mama Dorcas Membe wakiangalia tanzanite iliyochongwa saizi mbalimbali tayari kwa mauzo.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
Na Anna Nkinda –
Colombo, Sri Lanka
Mkutano wa
22 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola umefunguliwa leo mjini Colombo nchini Sri Lanka kwa mara ya
kwanza na mtoto wa Malkia wa Uingereza Price Charles bila ya kuhudhuriwa na
Malkia Eizabeth wa Pili ambaye ni mkuu
wa Jumuiya hiyo.
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahinda
Rajapaksa Theatre Prince Charles alisema viongozi hao wanakutana ikiwa ni mwaka mmoja tangu kusainiwa kwa
makubaliano ya kuboresha utendaji kazi wa jumuia hiyo hivyo basi makubaliano
hayo yawaongoze ili watakapokutana tena wasijadili changamoto zinazowakabili
bali ni jinsi gani wameweza kufanikiwa.
Aidha
atika mkutano
kama huo wa mwaka 2011 uliofanyika mjini Perth nchini Australia Malkia
Elizabeth alitangaza kuanzishwa kwa mfuko wa Diamond Trust Jubilee ambao
utawanufaisha
nchi wanachama wa Jumuia ya Madola. Tangu kuanzishwa kwa mfuko huo
umeweza kuwafikia na kuwasaidia watu , mashirika, wafanyabiashara
na Serikali za nchi wanachama.
“Kama mlivyosikia mfuko
huu unafanya kazi kubwa mbili ambazo ni kutibu
na kuzuia ili kuepukana ugonjwa wa upofu
wa macho pia kuna programu mpya ya
viongozi vijana inayotambulika kama Her Majesty’s Diamond Jubilee .
Miradi hii itasaidia
kubadilisha maisha ya watu mamilioni katika
nchi za Jumuia ya Madola ila haitaweza
kufanikiwa kama nyinyi hamtaweza kushiriki na kuendelea kuunga mkono mipango yote hii miwili”, alisema Prince
Charles .
Akiwakaribisha viongozi na wageni
waliohudhuria mkutano huo Rais wa Sri Lanka
Mahinda Rajapaksa alisema hivi sasa nchi
nyingi Duniani zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali
ngumu ya uchumi na kuziomba nchi wanachama wa jumuia hiyo kujadili kwa pamoja jinsi
gani wanaweza kukabiliana na hali hiyo katika nchi zao.
Rais Rajapaksa alisema , “ Sisi nchi wanachama wa Jumuia ya Madola tuangalie jinsi tunavyoweza kujadili vitu vinavyozuia kuleta maendeleo kwenye nchi zetu katika mambo ya siasa na uchumi bila ya kuwasahau wanawake na watoto .
Hata kama suala la uchumi litachukua nafasi tusiwasahau watu wetu, mtaji wa kutosha wa mtu unaisaidia nchi kufanikiwa na kuweza kukuwa ni muhimu watu waweze kuwasiliana katika nchi wanachama na uweza kutimiza malengo yetu.
Mkutano huo ambao
umeudhuriwa na wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa 41 kati ya nchi wanachama
52 akiwemo Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na mkewe Mama Salma
Kikwete unafanyika katika nchi ya Sri Lanka iliyopo barani Asia ikiwa ni baada
ya miaka 24 kupita tangu ufanyika kwa mkutano mkubwa kama huo.
No comments:
Post a Comment