Dar es Salaam. November 20, 2013.
PRECISION Air (PW) predicts
a rosier future in the years ahead with full implementation of the company’s
five-year strategic plan as approved by the company’s board, the Precision
Air's Board Chairman Michael Shirima said.
Speaking during the
company’s Annual General Meeting in Dar es Salaam yesterday, Shirima said the
company’s half year results(unaudited) for the period April to Sept indicates a
very positive outlook with the actual results
in line with the strategic plan,
Shirima said the
company is now focused to remain a profit making company even after posting a
Tshs 30 billion loss during the year ending March 31st 2013.
“Precision Air PLC has
weathered the storm of the past few years and remained intact amid challenging
environment of soaring jet fuel prices and slowdown of the global economy.
“Amid this challenging
environment, Precision Air recorded a loss of Tshs 30 billion for the year
ending March 31st 2013. Prior to this loss, the company had posted
an average of a net profit margin of 4 per cent for the preceding seven years
from 2006,” he said.
He said during that
period, the company’s total assets increased more than ten-fold from Tshs 23
billion in 2006 to Tshs 276 billion as on March 31st 2013.
“The growth of assets
was at par with the growth of the company’s capacity to airlift more
passengers. From moving 340,000 passengers in 2006 to 896,000 passengers in
2013 is not a small achievement. Indeed moving a total of close to 5 million
passengers over this period, all arriving at their respective destinations in
“one piece” is an enviable feat.
“Unfortunately, growth in the number of
passengers did not translate into profitability growth for reasons some of
which are pointed out below. The reported loss in 2013 brings down the average
net profit margin for the past 8 years to just one (1) per cent,” he added.
Shirima said
businesses with such narrow profit margins are highly sensitive to external
shocks affecting either revenue stream or cost elements.
“This is further complicated by the currency mismatch
Precision Air’s cash flow: revenues are mainly denominated in local currency
while larger percentage of costs (fuel and maintenance) is in foreign currency.
For example, a large part of Precision Air’s income is in shillings, while most of the
expenditure is in foreign currency (aircraft purchase, spare oil and large
repairs), therefore that possibility of losses arising reductions in the value
of the Tanzanian shilling compared to the American dollar,” he said.
He said the company’s
management foresaw these challenges and oncoming storms and acted proactively
to steer the company clear of turbulences adding that one of the steps deployed
was seeking long-term capital inviting new shareholders through Initial Public
Offer (IPO) and subsequently listing ordinary shares on the Dar es Salaam Stock
Exchange (DSE) in 2011.
“We did not succeed in
raising the amount we needed and this shortage roused many problems. The lack
of the capital expected put the Airline in a compromising position because the
aircrafts had already been ordered in advance since aircraft orders require
earlier placements and fifteen percent (15%) deposit of the price of these
aircrafts was paid.
“Cancellation of the
aircraft orders would have attracted heavy penalties and also slowed the
company's growth plans. As a result, the company experienced pressure on its
cash flow and eroded the company profitability but despite the above, the value
of shares in the DSE market, although rarely traded, have held steady at a
price of Tshs 475 per share.
Shirima said external
factors played part in this dismal performance, but admitted that there were
some internal manageable factors that had a significant share on the reported
results.
“After thorough
performance review for the past few years, the Board has noted key possible
source of trouble. These are: inefficient network, costly fleet type, low
productivity, lack of cost control and un-optimized ancillary revenue
opportunities.
“As a result, the
Board has appointed Deloitte & Touche to dig further into the performance
of the company, and we awaiting their report which will determine way forward.
Furthermore, the Board made significant change in management and is optimistic
that these problems presents an opportunity to drive back the company to
profitability for the days ahead.
He said his company is
currently pursuing other means to raise long-term capital in order to meet
expected huge capital commitments, some of which were postponed during the last
two years.
Shirima noted that
rationalization of the airline’s networks and fleet will be done by reviewing
current situation and utilization of sub-optimal capacity which was averaging
below 65 per cent for the past eight years.
“This will include
phasing out costly fleet and introducing single isle jets three years from now.
Such jets have belly capacity to also increase more revenue from cargo,”
He said Revenue
enhancement opportunities will focus on key revenue drivers: passenger revenue
– yield improvement and fuel surcharge improvement, excess baggage – tighter
control to improve collection, cargo – increase rates, and ancillary revenues –
third party aircraft maintenance and various advertisements.
“Other measures are aimed at business
consolidation and re-thinking of business model given the external competitive
environment. More importantly value enhancement will involve optimal deployment
of existing assets to increase cash flow, improving operational efficiency, and
reduce cost of financing. Cost control measures will not compromise fleet
safety.
He said successful
implementation of the above measures, coupled with securing long-term capital
will put the company back into profitability path and reward shareholders for
the patience endured during the turbulence period.
Precision Air kujiimarisha na mpango mkakati wa
miaka mitano
Na mwandishi wetu
SHIRIKA la Ndege la Precision Air limejipanga
kujiimarisha zaidi katika miaka michache ijayo baada ya utekelezaji wa mpango
mkakati uliopitishwa na bodi ya shirika hilo wa miaka mitano, Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Precision Air Michael Shirima amesema.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka jijini Dar
es Salaam jana, Shirima alisema matokeo ya shirika ya nusu mwaka kwa kipindi
cha Aprili mpaka Septemba kimeonyesha matarajio chanya ya kuwa na matokeo
mazuri yatokanayo na mkakati huo.
Shirima alisema shirika sasa limelenga kubaki kuwa
shirika linalotengeneza faida zaidi licha ya kupata hasara ya shilingi bilioni
30 katika kipindi cha mwaka unaoishia Machi 31, 2013.
“Shirika la Precision Air PLC lilipata changamoto
mbali mbali katika miaka michache iliyopita na kubaki kuwa imara licha ya
kukumbana na changamoto za bei ya mafuta na kuanguka kwa uchumi duniani.
“Kutokana na changamoto hizi, Precision Air ilipata
hasara ya shilingi bilioni 30 kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Machi 31,
2013. Kabla ya hasara hii, shiriki liliweza kupata kadirio la faida ya asilimia
4 katika kipindi cha miaka saba kuanzia mwaka 2006,” alisema Shirima.
Alisema wakati wa kipindi hicho, mali za shirika
ziliongezeka zaidi ya mara kumi kutoka shilingi bilioni 23 mwaka 2006 mpaka
bilioni 276 ilipofika Machi 31, 2013.
“Ongezeko la mali za shirika lilienda pamoja na kukua
kwa uwezo wa shirika kubeba abiria wengi zaidi. Kutoka kusafirisha abiria
340,000 kwa mwaka 2006 mpaka abiria 896,000 kwa mwaka 2013 siyo mafanikio
madogo. Kufikia jumla ya abiria milioni 5 kwa kipindi hiki, wote wakifika
katika maeneo yao “kwa amani” ni suala la kujivunia.
“Kwa bahati mbaya, kuongezeka kwa idadi ya abiria
haukuliwezesha shirika kuongeza faida kwa sababu ambazo zimeelezwa hapa chini.
Hasara iliyopatikana mwaka 2013 imesababisha kushuka kwa faida katika miaka
nane iliyopita mpaka asilimia moja,” aliongeza.
Shirima alisema kuwa biashara zinazokuwa na faida
ndogo kiasi hicho utokana na sababu zitokazo nje zinazoathiri aidha mapato ya
shirika au gharama za uendeshaji.
“Hali hii imekuwa mbaya zaidi kama kuna kutokuwiana
kwa mapato na matumizi (currency mis-match). Kwa mfano sehemu kubwa ya
mapato ya Precision Air ni katika shilingi wakati sehemu kubwa ya matumizi ni
fedha za kigeni (ununuzi wa ndege, vipuri mafuta na mategengenezo makubwa),
hivyo kuwa na uwezekano wa hasara inayotokana kupungua kwa thamani ya Shilingi
ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya kimerikani,” alisema.
Alisema kuwa uongozi wa shirika ulitambua vikwazo na
changamoto hizo mapema na kuchukua hatua za awali kukabiliana nazo ili
kuinusuru kampuni na kuongeza kuwa njia mojawapo kubwa ya jitihada hizo ni
kutafuta mtaji wa muda mrefu kupitia uuzaji wa Hisa kwa Umma kwa Mara ya Kwanza
na hatimaye kuzioredhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) mwaka
2011.
“Hatukuweza kufanikiwa katika kuongeza kiasi
tulichokihitaji na upungufu huu ukaleta matatizo mengi. Kutopatikana kwa mtaji
uliotarajiwa kuliliweka shirika mahali pabaya kwani ndege zilikwisha agizwa na
kulipiwa fedha za awali na kiasi cha asilimia 15 cha bei za ndege hizo
ililipwa”
“Haingekuwa busara kujitoa katika kununua ndege kwani fedha za amana zingepotea
na uimarishaji wa shirika ungeadhiriaka kwa kukosa ukuaji. Na matokeo
yake ni shirika lilipata shinikizo la mtiririko wa fedha (cash flow) na
upatikanaji wa faida. Pamoja na hayo thamani ya hisa katika soko (DSE)
haikuporomoka kwa kuwa zimesimamia kwenye Tshs 475 kwa kila hisa,” alisema
Shirima.
Shirima alisema kuwa ni kweli sababu zilizo nje ya
kampuni zimechangia kuwa na matokeo hafifu ya biashara. Ila ni hekima kukubali
kuwa kulikuwa pia na sababu za ndani ya kampuni ambazo zimechangia kwa kiasi fulani
kutufikisha hapa.
“Baada ya uchambuzi wa kina wa utendaji wa kampuni,
Bodi imebaini maeneo yafuatayo kuwa inawezekana ndicho kiini cha kudorora kwa
ufanisi. Maeneo hayo ni mtandao wa safari usio na ufanisi, ndege zenye gharama
kubwa ya uendeshaji, tija hafifu, kukosekana udhibiti wa matumizi na udhaifu wa
kufuatilia vyanzo mbadala vya mapato.
“Tumepata fundisho na hivyo Bodi imefanya mabadiliko
makubwa ya kiuongozi ikizingatiwa kuwa haya matatizo yameonesha fursa ya
kurudisha biashara katika mwelekeo wa faida siku zijazo,” aliongeza.
Aidha, alisisitiza kuwa hivi sasa shirika hilo liko
kwenye mazungumzo ya kupata mtaji wa muda mrefu ili kukidhi utekelezaji wa
majukumu yaliyoahirishwa miaka miwili iliyopita.
Shirima alibainisha kuwa uwiano wa mitandao ya
safari zilizopo utafanyika kwa kuangalia hali iliyopo sasa yakibiashara na
utumiaji wa ‘sub-optimal capacity’ ambao ulipungua kwa asilimia 65 katika
kipindi miaka nane iliyopita.
“Hii itajumuisha uondoaji wa ndege zenye gharama kubwa
na kuleta ndege kubwa aina ya Jet miaka mitatu kuanzia sasa. Ndege hizi
zinauwezo mkubwa wa kubeba abiria na kuongeza mapato kutokana na mizigo,”
alisema Shirima.
Alisema fursa za kuongeza mapato zitajikita kwenye
vyanzo vikuu, ambavyo ni: nauli – kuboresha tija na tozo ya ziada kwa ongezeko
la bei ya mafuta; mizigo ya ziada – udhibiti ili kuongeza makusanyo; mizigo ya
jumla – kuongeza viwango vya tozo; na mapato mbadala – matengenezo ya ndege za
kampuni nyingine na matangazo.
Njia nyingine zitakazotumika ni kupitia upya muundo wa
biashara kwa ujumla na kufikiria upya utayari wake katika mazingira ambayo
ushindani ni thabiti. Muhimu zaidi ni kwamba kuongeza thamani ya biashara kwa
wamiliki wa kampuni kutahusisha matumizi mahususi ya rasilimali zilizopo katika
kuongeza faida, kuongeza ufanisi wa kiutendaji, na kupunguza gharama ya mtaji.
Hata hivyo, udhibiti wa gharama kamwe usifikie hatua ya kudhoofisha usalama wa
vyombo vya usafiri.
Alisema mafanikio ya utekelezaji wa yaliyoainishwa
hapo juu, pamoja na upatikanaji wa mtaji utaiwezesha kampuni kupata faida na
hivyo kuwafaidisha wanahisa waliovumilia katika kipindi hiki cha dhoruba na
mitetemo ya kibiashara.
No comments:
Post a Comment