Msanii wa kundi la sanaa kutoka Bariadi akicheza na
nyoka aina ya Chatu wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi –Lamadi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi
ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Bariadi Lamad.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John
Pombe Magufuli(watatu kushoto),Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na viongozi
wengine w akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi
wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko enelo la Old
Maswa mkoa mpya wa Simiyu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa
kumbukumbu katika eneo la Old Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa
barabara ya kilometa ya Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani
Simiyu.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(pembeni ya Rais
kulia) pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi ujenzi
wa Barbara ya Bariadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko eneo la Old
Maswa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
Bwana Saguda Kasili mlemavu ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali
leo wakati aliposimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
Bwana Saguda Kasili mlemavu ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali
leo wakati aliposimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe
kuzindua rasmi Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi, Mkoa
wa Simiyu leo.Weninge katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na
Madini Mh. Steven Masele, Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge(wapili kushoto),Paroko
wa Nkololo Padri Paulo Fegan(wanne kushoto) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Pascal Mabiti.(Picha na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment