WABUNGE WA EALA KUTOKA TANZANIA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE, WASISITIZA MAZUNGUMZO KUTATUA MIGOGORO
WABUNGE wanaoiwakilisha Tanzania
katika Bunge la Afrika Mashariki wamesema suluhisho la matatizo ya nchi za
Maziwa Makuu yatapata ufumbuzi wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa
meza moja kwa pande zote husika na kufanya mazungumzo ya kuleta amani.
Hayo yalisemwa leo
jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge hao, Adam Kimbisa wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo pia alipongeza
hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alioitoa Bungeni Dodoma Novemba 7 mwaka huu juu
ya Jumuiya hiyo.
“Sisi tunaamini amani ni
jambo la msingi katika Afrika Mashariki na hasa katika nchi zilizo katika
Maziwa Makuu. Tunawapongeza wanajeshi wetu na wanajeshi Maalum wa Umoja wa
Mataifa kwa kazi nzuri walioifanya iliyowezesha mafanikio kupatikana” alisema.
Akielezea juu ya baadhi
ya nchi wanachama wa EAC ambao ndio waanzilishi wa vurugu mbalimbali na
migogoro Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tanzania imekomaa kisiasa hivyo hawawezi
kuwaondoa wale wanaoleta chokochoko kwa kuwa dawa ni kuzungumza na sio kuwatoa.
Mtangamano
Aidha Kimbisa amesema misingi
ya Utengamano wa kiuchumi ikijengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo wananchi
wote wa Afrika Mashariki watafaidika na hivyo suala la kuruka hatua yoyote ni
jambo lisilokubalika.
“Tunaungana na kauli ya
Rais kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa Mtangamano
zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hatua yoyote. Hatua ya kwanza ni
Umoja wa Forodha inafuata soko la Pamoja kasha Umoja wa Fedha na hatimaye
shirikisho la Kisiasa” alisema.
Alisema hadi sasa ni
hatua mbili zilizotiwa saini na mchakato wa kuweka saini Umoja wa fedha
unatarajiwa kutiwa saini baada ya kikao cha Juu cha Marais kinachotarajiwa
kufanyika mjini Kampala Novemba 30 iwapo masuala yote muhimu ya mchakato huo
yatakuwa yamekamilika.
“Jambo la msingi ambalo hata Mkataba wa
Uanzishwaji wa Jumuiya imesema wazi kwamba Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi
kwa manufaa ya wananchi na isiwe ya viongozi. Wananchi washirikishwe katika kila
hatua na kila ngazi ili iweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao”
alisema.
Kuhusu VISA alisema kuwa wao wanaruhusu nchi
nyingine kuendelea lakini Tanzania bado hawajafikia muafaka kwa kuwa
wanaangalia maslahi ya nchi kwanza. Katika Hatua nyingine, Wabunge hao
walimpongeza Rais Kikwete kupeleka kikosi cha Wanajeshi katika Brigedia Maalum
iliyoundwa na Umoja wa Mataifa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika
Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba
yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao,
Shy-Rose Bhanji.
Kimbisa akizungumza na wanahabari Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.
wanahabari wakifuatilia hotuba hiyo..
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika
Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba
yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao,
Shy-Rose Bhanji. Kulia ni Mkurugezni Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika
Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akiteta jambo na Katibu wake,
Shy-Rose Bhanji.
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki,
Shay-Rose Banji na Adam Kimbisa wakitoka katika Ukumbi wa MAELEZO Dar
es Salaam leo baada ya kuzingumza na wana habari.
No comments:
Post a Comment