Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dk. Batilda Burian akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
katika maonesho ya Kikanda ya Wajasiriamali yananayojulikana kama Jua Kali/
Nguvu Kazi exhibition na kufanyika jijini Nairobi juzi.
NSSF
yapongezwa Nguvu Kazi Exhibition 2013
Mwandishi
Wetu
BALOZI wa Tanzania nchini Kenya, Dk Batilda Buriani, amelipongeza
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa harakati chanya za kuwakomboa
wajasiriamali wakubwa na wadogo waliopo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC).
Dk Buriani alitoa pongezi hizo kwa NSSF na Taasisi
kutoka Tanzania chini ya Wizara ya Afrika Mashariki na Wizara ya Kazi (MKURABITA,
TFDA na TanTRADE), hivi karibuni baada ya kushiriki Maonesho
ya Wajasiriamali ya Jua Kali/ Nguvu Kazi Exhibition.
Nguvu
Kazi Exhibition 2013 yalifanyika jijini Nairobi,
ambako NSSF ilishiriki kwa mara ya nne, kwa nia ya kuwafikia wajasiriamali ili
kuwaongezea elimu kuhusu mafao ya shirika lake, yakiwemo ya matibabu, uzazi,
kuumia kazini na Mikopo ya Saccos.
Dk
Buriani alikiri kuvutiwa na harakati chanya zinazofanywa na NSSF, hivyo
hakusita kulipongeza huku akilitaka kuongeza kasi ya kuwafikia wajasiriamali na
wakulima, ili kuhakikisha wanaelimishwa na kutumia fursa zinazopatikana kwa
kujiunga na shirika hilo.
Kwa
upande wake Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume, alisema ili kutanua
fursa miongoni mwa wajasiriamali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, shirika lake
linatambua umuhimu wa kutumia maonesho Jua Kali/
Nguvu Kazi Exhibition kuwafikia.
“NSSF
imeshiriki Jua Kali/ Nguvu Kazi Exhibition kwa mara ya nne, lengo likiwa ni kutanua
wigo wa huduma za shirika nje ya Tanzania, ikiwamo kuongeza idadi ya wanachama wa
mafao na huduma mbalimbali za NSSF,” alisema Chiume.
Chiume
aliongeza kuwa, NSSF linatoa mafao saba kama tamko la Shirika la Kazi la
Kimataifa (ILO) linavyotaka, ambako kwa niaba ya shirika aliwatangazia wadau wa
sekta binafsi wakiwamo wajasiriamali na wakulima ‘Fursa’ mbalimbali
zinazopatikana kwa kujiunga NSSF.
NSSF
pia imetoa ‘Fursa’ kwa Watanzania waishio Ughaibuni kujiunga na shirika
kwa mfumo wa WESTADI na kuwawezesha kupata mafao ya matibabu kwa Wategemezi
wanne waliopo Tanzania na usafirshaji wa mwili mwanachama anapofariki nje ya
nchi.
No comments:
Post a Comment