Utangulizi
Upungufu wa vitamini na madini ni mojawapo ya matatizo
makubwa ya kilishe yanayowaathiri hasa watoto na wanawake walio katika umri wa
kuzaa hapa Tanzania. Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii (Demographic and Health Survey) za mwaka
2010 zinaonesha kuwa hapa Tanzania upungufu wa vitamini A unaathiri asilimia 33
au theluthi moja ya watoto walio chini ya miaka mitano na asilimia 37 au zaidi
ya theluthi moja ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Upungufu wa madini
chuma unaathiri asilimia 59 au zaidi ya nusu ya watoto wadogo na karibu
asilimia 41 au karibu ya nusu ya akina mama wajawazito, na pia upungufu wa madini
joto unakadiriwa kuathiri asilimia 7 ya Watanzania. Utoaji wa matone ya
vitamini A kwa watoto ni njia mojawapo ambayo inatumika kupunguza madhara ya
upungufu wa Vitamini A.
Kwa
kuanzia tuangalie chanzo cha upungufu wa vitamini A
.
• Vitamini A ni mojawapo ya vitamini isiyotengenezwa na
mwili na hivyo ni lazima itokane na vyakula viliwavyo na binadamu na wanyama
• Vyakula vyenye vitamini A kwa wingi
– Mboga na matunda hasa yenye rangi ya kijani na njano
– Samaki
hasa dagaa
– Mafuta
ya mawese
– Maini
Sababu
za Upungufu
•
Ulaji
duni usiokidhi mahitaji ya Vitamini A mwilini
•
Unyonyeshaji
watoto maziwa ya mama usiokidhi mahitaji ya mtoto (Sub optimal breastfeeding)
•
Magonjwa ya mara kwa mara
•
Utunzaji duni wa makundi husika
•
Mgawanyo
mbaya wa rasilimali (usiotoa kipaumbele kwa makundi maalum yaani kina mama na
watoto
Waadhirika wakuu:
• Watoto
walio katika umri wa chini ya miaka mitano
• Wanawake
walio katika umri wa uzazi.
• Asilimia
33 ya
watoto walio katika umri wa chini ya miaka 5 wana upungufu wa vitamini A
• Asilimia 37 ya akina mama walio katika umri wa kuzaa wana upungufu wa vitamini A
Madhara
ya Upungufu wa vitamini A
• Kutokuona
vizuri kwenye mwanga hafifu
• Upofu
• Maradhi ya mara kwa mara kutokana na kupungua kwa kinga
ya mwili
• Vifo
hasa vya watoto
• Kushuka
kwa elimu
• Kupungua
kwa tija (maradhi yanayotokana na upungufu wa vitamini A huifanya familia
husika kutumia rasilimali fedha na muda mwingi kwa ajili ya kumtibia mtoto).
Njia zinazotumika kupambana na
tatizo
• Unyonyeshaji
sahihi wa watoto
• Ulaji
wa vyakula vyenye virutubishi hasa vya
vitamin A kwa wingi na vya mchanganyiko
• Ulaji
wa matunda na
mboga za majani kwa wingi (Vyenye rangi ya kijani kibichi na
njano)
• Kutoa matone ya vitamini A kwa watoto walio katika umri
wa miezi 6 hadi miaka mitano.
Utoaji
wa matone ya vitamin A
Zoezi la utoaji wa matone ya vitamini A hutolewa kwa
watoto walio katika umri wa miezi 6 hadi miaka mitano mara mbili kwa mwaka
(Juni na Desemba). Zoezi hili hufanyika
sanjari na utoaji wa dawa za minyoo, dawa hizi hutolewa kwa watoto wenye umri
wa mwaka 1 hadi miaka 5.
Watoto wa umri wa miezi 6 hadi miezi 12 hupewa kidonge
chenye IU 100,000
Watoto wa umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano hupewa
kidonge chenye IU 200,000.
Matone yanatolewa katika vituo vya afya na vituo vya muda
(mobile clinics). Lengo la kufanya hivyo
ni kutaka kuwafikia watoto wengi zaidi.
Kwa Tanzania zoezi limekuwa likiwafikia watoto zaidi ya
asilimia 80.
Changamoto zinazolikabili zoezi
• Upatikanaji
wa takwimu sahihi dhidi ya walengwa ili kupata matone ya vitamini A ya kukidhi
mahitaji ya walengwa.
• Upatikanaji
kwa takwimu za Idadi ya watoto waliopata matone ya vitamini A na kuzifikisha
taarifa hizo katika ngazi husika kwa wakati ili ziweze kufanyiwa maamuzi.
•
Kuweza kuwafikia walengwa wote hasa
maeneo ambayo ni magumu kufikika – kisiwani, milimani nk.
Wazazi
na walezi wanapaswa kufahamu nini? Ujumbe muhimu
Kila
mzazi / mlezi wa mtoto aliye chini ya umri wa miaka 5 anapaswa kufahamu umuhimu
wa vitamini A kwa ukuaji, maendeleo mazuri, afya na uhai wa mtoto. Ni muhimu
wazazi/ walezi wafahamu kuwa vyakula tunavyokula
havikidhi mahitaji ya vitamini A mwilini kwa watoto, watoto hula kiasi kidogo cha vyakula vyenye vitamini
A wakati mahitaji yao
ni makubwa. Hivyo hawana budi
kupewa matone ya vitamini A mara mbili kila mwaka ili kukidhi mahitaji
hayo. Pia wanapaswa kufahamu wakati na
mahali ambapo zoezi la utoaji wa matone ya vitamini A hufanyika ili waweze
kuwapeleka watoto wao kila baada ya miezi sita.
No comments:
Post a Comment