WanaCCM
nchini tuko katika mstari wa mbele kuisimamia Serikali yetu kwa mujibu wa Ilani
ya CCM ya mwaka 2010-2015 sura ya Tisa; Inayokitaka Chama kuisimamia Serikali
yake.
Kwa
pamoja tunaungana na kupinga kwa nguvu zote mambo yafuatayo;
1. Ubadhirifu
unaofanywa katika Serikali za Mitaa nchini unaozifanya Halmashauri nyingi kujirudiarudia
kupata hati chafu na zenye mashaka, inayosababisha hasara na manung’uniko kwa
wananchi.
2. Utelezaji duni
wa baadhi ya miradi ya maendeleo unaopelekea kuwepo kwa huduma duni na
zisizokidhi thamani ya fedha na matakwa ya kitaalamu. Hii inaashiria uwepo wa
Rushwa na ubadhirifu wa fedha kwa baadhi ya miradi ya maendeleo.
3. Ucheleweshaji wa
maslahi na stahiki za watumishi wa Umma kunakopelekea kuwa wavunja moyo na ari
watumishi, katika kutekeleza majukumu yao na hivyo kusababisha kutokea kwa
migomo ya mara kwa mara kufuatia uzembe katika kuwapatia haki zao, kinyume na
misingi ya utawala bora.
4. Gharama kubwa ya
uendeshaji wa shughuli za Serikali na Taasisi zake ikilinganishwa na gharama
zinazotumika kwenye miradi ya maendeleo na uboreshwaji wa huduma za jamii kwa
wananchi.
5. Usimamizi mbovu
wa Operation mbali mbali za Serikali zenye nia njema kwa Taifa. Mfano
Operasheni kuhamisha wafugaji na Operasheni Tokomeza; Zina nia njema lakini
usimamizi wake umekuwa mbovu hata kupelekea kuvuruga nia yake njema kwa Taifa.
6. Kushindwa na
Kuchelewa kutatua baadhi ya Kero sugu kwa Wananchi kama malalmiko mbali mbali
ya wakulima (mfano mbolea za minjingu kutofanya vizuri kwa asilimia kubwa,
matatizo ya wakulima wa pamba na korosho nk.) na wafugaji; Rushwa zilizokithiri
katika sehemu mbali mbali za utoaji wa huduma kwa wananchi na ucheleweshwaji wa
fadha za miradi ya maendeleo nk.
Katibu Mkuu wa
CCM daima amekuwa akikemea kwa nguvu zote madhaifu yote tuliyoyataja hapo juu
na sisi kama Wenyeviti wa CCM Mikoa yote Tanzania. Tunaitaka Serikali ichukue
hatua za haraka katika kurekebisha madhaifu hayo. Viongozi na watendaji wengine
wote wa Serikali, walioonesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao, na
ambao walipewa wito na wengine ambao wanatakiwa kupewa wito; wa kuhudhuria
mbele ya Kamati Kuu ya CCM wachukuliwe hatua zinazostahili. Tunawakumbusha
viongozi wa Serikali watambue kuwa Chama cha Mapinduzi kinaisimamia Serikali
kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka
2010-2015 Sura
ya Tisa.
_______________________________________________
Mgana Izumbe
Msindai – Mwenyekiti wa Wenyeviti Mikoa
______________________________________________________
Haji Juma
Haji – Makamu Mwenyekiti Wa
Wenyeviti Mikoa
______________________________________________
Lucas Ole Mukusi
– Katibu wa Wenyeviti Mikoa
TUNAWASILISHA
No comments:
Post a Comment