Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya Pamoja
na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini
Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Freddy Maro)
Na Freddy Maro
Washirika wa Maendeleo wa Tanzania wakiwemo baadhi ya
mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa na mashirika ya Kimataifa wameelezea
kuridhishwa kwao na juhudi za Serikali ya awamu ya Nne ya Tanzania inaoongozwa
na Rais Dkt.Jakaya Kikwete, katika mapambano dhidi ya Rushwa nchini.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
mara baada ya kukutana na baadhi ya Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya
kimataifa ikiwemo Banki ya Afrika,Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la
Kimataifa(International Monetary Fund) ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.
“Yaliyojitokeza katika mkutano huu ni wao kutambua juhudi za
serikali yetu kuimarisha vita dhidi ya rushwa ka kuimarisha taasisi
zinazohusika moja kwa moja kwa kuziongezea bajeti na kuajiri wafanyakazi wenye
uwezo na ujuzi wa kutenda kazi kwa weledi.Ofisi hizi ni pamoja na TAKUKURU
yenyewe, ofisi ya mwendesha mashtaka, Mahakama, sekretarieti ya maadili ya umma
na polisi,” alisema Balozi Sefue.
Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuwa washirika hao wa maendeleo
wamefurahi kutambua kwamba Serikali imeongeza idadi ya watumishi wa umma
wanaofanya kazi katika taasisi zinazohusika na vita vya rushwa nchini na
kuboresha utendaji baada ya kupata mafunzo na kwamba miundo mbinu ya taasisi
hizi ikwemo majengo ya ofisi na vitendea kazi vimeimarishwa.
Balozi Sefue
aliongeza kusema kuwa washirika hao wa maendeleo wamekuwa wawezeshaji wakuu wa
taasisi zinazopambana na rushwa nchini kwa kuzichangia kwa fedha na kugharamia
mafunzo ya baadhi ya watumishi wa taasisi hizo na kwamba katika mkutano wa leo
wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania katika vita dhidi ya Rushwa
kwa kuisaidia serikali kuimarisha mifumo, sheria, taratibu na kutoka mafunzo
kwa watumishi.
Baadhi ya Washirika wa Maendeleo waliohudhuria mkutano wa
Katibu Mkuu kiongozi ni pamoja na wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya EU,
Balozi wa Unigereza nchini, Balozi wa Canada,Balozi wa Norway,Balozi wa
Finland, Balozi wa Denmark,Balozi wa Ujerumani, Balozi wa Ireland, Balozi wa
Sweden, Mwakilishi wa Ubalozi wa Japan, Mwakilishi wa Benki wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika, mwakilishi wa Benki ya Dunia na Mwakilishi wa Shirika la
Fedha la Kimataifa(IMF).
No comments:
Post a Comment