Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wakitoa maelezo kuhusu shughuli wanazozifanya walipotembelewa na wananchi mbalimbali waliohudhuria maonyesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye viwanja vya Betrasi mjini Unguja.
Na Irene Mark, Zanzibar
KATIKA kukabiliana na uhaba wa Wakaguzi wa Marubani
wa Ndege, Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeajiri wataalam watatu wa kada
hiyo kwa mwaka 2013.
Ofisa Habari wa Mamlaka hiyo, Ally Changwila alisema kuwa kuajiriwa kwa wataalam hao kunaongeza idadi
yao na kufikia sita kwa sasa.
Ofisa huyo alisema hayo wakati
wa maonyesho ya siku tatu ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar
yaliyomalizika jana visiwani humo.
Kwa mujibu wa Changwila kada
hiyo ya wakaguzi wa marubani inakabiliwa na upungufu wa watumishi 12 ili
kufanikisha ufanisi katika eneo hilo.
Aliongeza kwamba changamoto
mbalimbali zinachangia eneo hilo kuwa na watumishi wachache ni gharama kubwa za
masomo ya kada hiyo nje ya nchi na uduni wa mishahara.
Awali alibainisha kwamba mwaka
2013 katika upande wa usajili wa ndege TCAA imesajili helkopta tatu mpya ambazo
sasa zinatumika kufanikisha shughuli za utafiti wa mafuta, gesi na huduma za
kukodi.
Alieleza majukumu muhimu ya
mamlaka hiyo kuwa ni udhibiti wa usalama, udhibiti uchumi katika eneo la anga
na utoaji wa huduma za uongozaji wa ndege.
No comments:
Post a Comment