JESHI LA ULINZI LA
WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo
: “N G O M E”
Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo :
DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex :
41051 DAR ES SALAAM, 20 Januari, 2014
Tele Fax :
2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti :
www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mujibu wa Kanuni za Majeshi ya
Ulinzi, Aya ya 7.01 Kifungu cha 13 Juzuu ya Kwanza (Utawala), amewapandisha Cheo
Maafisa Wakuu kutoka Kanali kuwa Brigedia Jenerali.
Aidha, Maafisa Wakuu hao ni:-
Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula,
Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas
Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray,
Kanali Emmanuel Peter Kapesa, Kanali Mwita Wambura Isamulyo, Kanali Francis
Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali
Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea
Msanja, Kanali Blasius Kalima Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali
Rajabu Goma Hanti, Kanali Ignas Beatus Mubofu, Kanali Dominic Basil Mrope,
Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko
Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge,
Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy
Philip Njelekela.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli
Ndomba kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange
amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo katika
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Luteni Jenerali Ndomba alisisitiza
kusimamia nidhamu na ueledi mambo ambayo ndiyo msingi wa mafanikio katika
utendaji wa Majeshi.
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P
9203, Dar es Salaam, Tanzania.
No comments:
Post a Comment