JESHI LA ULINZI LA
WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo
: “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo :
DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex :
41051 DAR
ES SALAAM, 04 Februari, 2014
Tele Fax :
2153426
Barua pepe :
ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti :
www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linapenda kuwataarifu kuwa tarehe 05
Februari 2014 Brigedi ya CHUI, ambayo
Makao Makuu yake yapo ‘Lugalo Military Barracks’ karibu na
hospitali ya Lugalo, itaazimisha miaka arobaini (40) ya kuanzishwa kwake. Mgeni wa heshima atakuwa aliyewahi kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Said
Kalembo. Sherehe hizo zitatanguliwa na michezo
mbalimbali kuanzia saa 2.00 asubuhi.
Kutakuwa na tukio la Brigedi kutoa vifaa
vya msaada katika Hospitali ya
Mwananyamala, saa 5.00 asubuhi. Baadae saa 10.30 jioni sherehe rasmi zitaanza na kumalizika saa 6.00 usiku.
Aidha, Waandishi wa Habari
wanakaribishwa katika sherehe hiyo kwenye viwanja
vya Lugalo hospitali ili kufanya ‘Coverage’.
Imetolewa
na Kurugenzi ya
Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P. 9203
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment