WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”
&
nbsp; Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu :
(022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.
TAARIFA YA
JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu
amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa
mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa
vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko
ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi
(SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara
kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa
Ruvuma.
Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi
Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,
aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan
Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa
kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna
msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na
aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa
Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu
wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora
Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi
mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi
wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .
Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa
Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi
Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu
wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda
kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama
Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda
Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa
Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa
Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni
aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi
Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,
aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa
Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa
Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa
Ilala.
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa
kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba
wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa
Jeshi la Polisi
No comments:
Post a Comment