Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua
jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William
Kallaghe(kushoto) alipokutana naye ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo
wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo(kulia)
akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel(katikati) na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA)
Bw. William Kallaghe(kushoto) jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda
(kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel(kulia) na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw.
William Kallaghe(katikati) jana jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel (kulia) akiagana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis
Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumza
yao jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya
Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda
(katikati) akiteta jambo mara baada ya kikao chao kumalizika, kulia Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo na kushoto ni Katibu Mkuu wa
Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe jana Dar
es Salaam.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijina, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, Katbu Mkuu wa Chama
cha Mchezo Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe na Mkurugenzi Msaidizi wa
Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda wakiwa katika p[icha ya pamoja mara
baada ya kumaliza kikao chao jana Dar es Salaam.(Picha zote na Frank Shija - Wizara
ya Habari).
Na Frank Shija - WHVUM
Viongozi wa vyama vya michezo nchini
wametakiwa kutmia fursa zilizopo kukutana na viongozi wa Serikali ili
kujadili kwa pamoja namna ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel alipokutana Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA)
Bw. William Kallaghe alipomtembele ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
Profesa Elisante alisema kuwa ni
vyema viongozi wa vyama vya michezo kushirikiana na Serikali katika kutafuta
namna ya kuendeleza michezo nchini badala ya kukaa na kulalamikia pembeni.
Aidha amesema kuwa milango iko wazi
kwa viongozi wa vyama vuya michezo kufika katika ofisi za Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo na kuongeza kuwa atafarijika sana akiona kasi ya
viongozi hao kutembelea Wizarani hapo ikiongezeka.
"Natao wito kwa viongozi wa
vyama vya michezo nchini wajenge utamaduni wa kushirikiana na Serikali kupitia
Wizara hii ili kutafuta namna na njia bora ya kuendeleza sekta ya michezo hapa
nchini badala ya kukaa pembeni na kuiilaumu Serikali, kwakweli hii si
sawasawa" Alisema Profesa Elisante.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama
cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe ameipongeza Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano ambao
wamekuwa wanautoa kwa vyama vya michezo hapa nchini na kusema kuwa hii inaleta
faraja kuwafanya kutokuwa wapweke.
Kallaghe aliongeza kuwa ni vyema
sasa viongozi wa vyama vya michezo wakatambua umuhimu wa kufanya kazi kwa
karibu na Serikali ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao
mbalimbali.
Aliongeza kuwa atahakikisha
anahamasisha viongozi wenzake kutumia fursa za kukutana na viongozi wa Serikali
ili kukaa meza moja na kujadiliana namna ya kuboresha sekta ya michezo hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment