KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Thursday, February 13, 2014

TIC YASAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI NA WAKUU WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.

 Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki wakati alipotembelea Banda la Kituo hicho kwenye Maonyesho ya Kongamano la Uwekezaji yaliyoanza jana kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (katikati) akisaini Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ,wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mmanza,Mh. Everist Ndikilo (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Yohana Balele (kushoto).Wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri.na Kulia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akibadilishana Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki mara baada ya kusainianiana na wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,jijini Mwanza jana.Shughuli hii imefanyika wakati wa Muendelezo wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa.
 Mmoja wa Wawekezaji waliopo ndani ya Kanda ya Ziwa,akiwasilisha jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akizungumza wakati alipokuwatana na baadhi ya wawekezaji wenye leseni za TIC (hawapo picnani) ,kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Jijini Mwanza jana.(Picha Zote na Othman Michuzi,Mwanza).

No comments: